logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Patanisho: Jamaa aishi kwa hofu ya mkewe kugura ndoa wakati wowote

Kemboi alilalamikia tabia ya mkewe ya kuhusisha wazazi wake katika masuala ya ndoa yao.

image
na Radio Jambo

Habari22 March 2022 - 05:37

Muhtasari


•Jecinta alisema hata kama bado anaishi na mumewe hakujakuwepo na amani kwenye ndoa yao ya mwaka mmoja kwa kipindi cha miezi miwili.

•Kemboi alieleza kwamba amekuwa akiishi na hofu ya kuwa huenda mkewe akaondoka wakati wowote.

Gidi na Ghost asubuhi

Katika kipindi chetu cha Gidi na Ghost asubuhi kitengo cha Patanisho mwanadada aliyejitambulisha kama Jecinta Wangari (21)  alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mumewe Dan Kemboi (27).

Jecinta alisema hata kama bado anaishi na mumewe hakujakuwepo na amani kwenye ndoa yao ya mwaka mmoja kwa kipindi cha miezi miwili.

Alifichua kwamba alikuwa amegura ndoa yake mnamo mwezi Januari baada ya kutofautiana na mumewe kuhusu malezi ya mtoto aliyepata na mwanamke mwingine.

"Ilikuwa suala la mtoto. Alileta mtoto mwingine niishi naye. Wazazi wangu hawakufurahia kwa sababu alikuwa mdogo. Mimi nilikuwa nimekubali. Wazazi wangu wakawa wanaongea sana nikaona nimpeleke kwa nyanyake. Hawakuwa wanafurahia nikilea mtoto... Mume wangu alikuwa ameenda kazi Nairobi, tulikuwa tunawasiliana tu kwa simu lakini hatukuwa tunongea vizuri. Niliuza kuku tu, vitu vingine nikaacha kwa nyumba. Baadae nilirudi," Jecinta alisimulia.

Jecinta alikiri kwamba hakufahamisha mumewe kuhusu mpango wake ya kupeleka mtoto kwa mama mkwe. Alieleza kwamba hakujakuwa na maelewano katika boma yao tangu aliporejea.

Kemboi alipopigiwa simu alilalamikia tabia ya mkewe ya kuhusisha wazazi wake katika masuala ya ndoa yao. Vilevile alieleza kwamba amekuwa akiishi na hofu ya kuwa huenda mkewe akaondoka wakati wowote.

"Sina shida yoyote lakini kama mtu akiumwa na nyoka huwa anakumbuka. Umekuwa ukitoroka kila mara tukikosana kidogo. Sasa siwezi kuamini.  Ndoa ni ya watu wawili sio wa wazazi. Siwezi kuwa naishi na hofu kila siku," Kemboi alisema.

"Amekuwa confused. Nilipokuwa naleta mtoto nilikuwa nimemwambia. Alienda akaambia wazazi kisha akapeleka mtoto nyumbani. Baadae akarudi, nilimwachia pesa kwa nyumba akazichukua na kuzitumia kurudi kwao," Kemboi aliendelea kusema.

Jecinta alimhakikishia mumewe kwamba ameamua kutulia katika ndoa na kuahidi kutotoroka tena.

Kemboi kwa upande wake alikubali kumpa mkewe nafasi nyingine huku akimwomba awe mtulivu na asihusishe familia yao katika ndoa.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved