Patanisho: Jamaa atuma fare mara tatu hadi kufuliza, mpenziwe harudi!

Muhtasari

•Collins alisema Sharon aligura ndoa yao ya mwaka mmoja na kuenda kwao Desemba mwaka jana baada yao kupoteza mtoto.

Ghost na Gidi
Ghost na Gidi
Image: RADIO JAMBO

Jamaa aliyejitambulisha kama Collins ,25, kutoka Siaya alituma ujumbe wa Patanisho akiomba kupatanishwa na mpenzi wake Sharon ,22, ambaye  alimtema bila kumweleza sababu.

Collins alisema Sharon aligura ndoa yao ya mwaka mmoja na kuenda kwao Desemba mwaka jana baada yao kupoteza mtoto. Alisema mkewe alirudi mwezi uliopita ila baada ya wiki chache akaondoka tena na kurudi kwao.

"Tulikuwa naye nyumbani wiki iliyopita. Nilimtumia nauli akuje akakataa. Aliniambia aliona shida kwangu hawezi kurudi. Aliniambia vile alienda nyumbani wazazi wake hawakutaka arudi kwetu," Collins alisimulia.

Collins alifichua kwamba bado hajajitambulisha rasmi nyumbani kwa kina Sharon. Alisema anahofia kwenda kwao kwani hajui ni tatizo lipi mashemeji waliona kwake.

"Naweza enda kwao nipigwe. Nataka aniambie shida ni gani ili niende nijitambulishe. Ananitumia jumbe na kunipigia simu. Nimetuma fare mara tatu. Nimetuma fare mara tatu hadi nikafuliza na hakuji," Alisema Collins.

Baada ya Sharon kupigiwa simu aliikata mara moja punde baada ya Collins kuanza kumwongelesha. Collins hata hivo alifungua roho hewani na kumsihi amrudie huku akidai kuwa anateseka.

"Sharon bado nakupenda sana. Ningependa urudi mpenzi wangu. Tuliza roho, maisha yangu yapo hatarini. Huwa naenda kazi nashinda na msongo wa mawazo. Hadi nashindwa kupika," Collins alisema.

Je, una ushauri gani kwa Collins?