Nilimpeleka kidosho wa mume wangu, kumtambulisha kwao-Mwanadada asimulia

Muhtasari
  • Katika kitengo cha patanisho Bi Lucy alituma ujumbe apatanishwe na mumewe Ng'ang'a wa miaka miwili, ambaye walitengana  baada ya mumewe kuoa mke wa pili
Gidi na Ghost asubuhi
Gidi na Ghost asubuhi
Image: RADIO JAMBO

Katika kitengo cha patanisho Bi Lucy alituma ujumbe apatanishwe na mumewe Ng'ang'a wa miaka miwili, ambaye walitengana  baada ya mumewe kuoa mke wa pili.

Kulingana na Lucy, alimpigia mumewe simu na ikapokelewa na mwanamke huyo,kisha akampeleka kwa mumewe.

"Naomba nipatanishwe na mume wangu ambaye tulitengana mwaka jana Agosti, baada yake kuoa mwanamke mwingine

Nilijua kwamba ana mwanamke mwingine baada ya kumpigia simu na mwanamke huyo kupokea simu yake,alikuwa ananitesa baada ya kuniacha mashambani, nilimpigia mwanamke huyo na kumleta nyumbani kwa mume wangu

Lakini nataka turudiane kwani washaachana na mwanamke huyo baada yake kumtesa kama alivyokuwa ananitesa."

Baada ya kufanya juhudi za kumfikia mumewe ili waweze kupatana na Lucy,mumewe alikata simu na wala hakuzungumza lolote.

Kwa mengi zaidi tembelea Radiojambo Youtube.