Patanisho: Jamaa apatikana akichat na mpango wa kando, adai alikuwa anatongozwa

Muhtasari

•Kibet alisema mkewe aligura ndoa yao ya miaka mitano baada ya kupata meseji za mpango wa kando kwenye simu yake.

•Alijitetea kwa kusema kuwa yeye hakuwa na nia mbaya na kudai kuwa mwanadada huyo ndiye alikuwa anamtongoza. 

Gidi na Ghost
Gidi na Ghost
Image: RADIO JAMBO

Katika kipindi chetu cha Gidi na Ghost asubuhi kitengo cha Patanisho jamaa aliyejitambulisha kama Kibet alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mkewe Mercy ambaye alidai alimuacha kufuatia mambo ya mpango wa kando.

Kibet alisema mkewe aligura ndoa yao ya miaka mitano baada ya kupata meseji za mpango wa kando kwenye simu yake.

"Alinipata nikichat na mpango wa kando kwa simu. Nilikuwa nimepatana na msichana ambaye alikuwa anatafuta kazi Eldoret, nikamwambia nikipata kazi nitamwambia. Kumbe alikuwa na mpango mbaya, alianza kunitumia meseji za mapenzi," Kibet alisema.

Alijitetea kwa kusema kuwa yeye hakuwa na nia mbaya na akadai kuwa mwanadada huyo ndiye alikuwa anamtongoza. 

Alikuwa anataka kunitongoza na sikuwa nataka hayo maneno. Mimi sikuwa najibu meseji zake. Mke wangu alipoenda nilipatana na huyo msichana na nikamuonya," Aliendelea.

Kibet alifichua kuwa amekuwa kwa ndoa na Mercy kwa miaka mitano na tayari wana watoto wawili ambao kwa sasa wanaishi na mkewe.

Alisema juhudi zake za kumrejesha mkewe nyumbani zimekuwa zikiangulia patupu kwani tayari amemfungia mawasiliano na familia yake imekataa kumwambia alipo.

Mercy alikosa kujibu licha ya Gidi kumpigia simu mara nne. Kibet alisema mkewe ni shabiki mkubwa wa Radio Jambo na huenda alikuwa anafuatilia kipindi.

Alichukua fursa hiyo kumhakikishia mkewe kuhusu mapenzi makubwa aliyo nayo kwake hewani na kumsihi arudi.

"Mercy nakupenda kama mursik. Wewe pekee ndo mke wangu, huyo msichana ni kama alikuwa anatafuta mwanaume sio kazi. Nakupenda sana," Alisema Kibet.