Nilikosana na mke wangu,baada ya shemeji yangu kumwambia nilimpachika mimba-Jamaa alia

Muhtasari
  • Kulingana na bwana huyo mkewe alimuacha baada ya dada ya mke wake kudai alimpachika mimba wwalipokuwa wanaishi pamoja
Gidi na Ghost
Gidi na Ghost
Image: RADIO JAMBO

Katika kipindi cha patanisho siku ya Ijumaa bwana Alfred alituma ujumbe ili apatanshwe na mkewe  Jacqueline baada ya kukosana mwka jana.

Kulingana na bwana huyo mkewe alimuacha baada ya dada ya mke wake kudai alimpachika mimba wwalipokuwa wanaishi pamoja.

"Nilikosana na mke wangu baada ya shemeji yangu ambaye ni dada ya mke wangu, kusema kwamba nilimpachika mimba,alikuwa nasomea kwangu ilhali sio mimi ambaye nilimpachika mimba

Pia alisema kwamba nimekuwa nikimtumia pesa lakini ni uongo, mke wangu aliniachia watoto, kisha akarudi kuwachukua na kuenda nairobi, aliniambia nitafuta mke mwingine kwani ameshaaolewa ilhali ni uongo hajaolewa," Alisimulia Alfred.

Baada ya kufikia mkewe alisema;

"Mbona alimpachika dada yangu mimba, nilimuita nyumbani aje aombe msamaha lakini alikataa,achana na mimi sitaki habari zake nimepata mwanamume mwingine naenda kwangu

Aliniambia watoto ni mzigo kwake nampea watoto ananirudishia, pia aliniambia nikimpata mwanamume mwingine nimwambie nimemwambia sasa,tafuta bibi mzae naye."

Kwa mengi zaidi tembelea Radiojambo Youtube

Gidi na Ghost
Gidi na Ghost
Image: RADIO JAMBO