"Kuja uchukue nguo ulizoninunulia!" Mwanadada amwagiza mumewe baada ya kufichua ana mke mwingine

Muhtasari

•Diana alisema ndoa yao ya miaka minne baada yake kutofautiana na mumewe kuhusu masuala madogo madogo.

•Collins alimwagiza mpenzi huyo wake wa zamani asonge mbele na maisha yake kwani yeye tayari yupo kwenye ndoa nyingine.

Gidi na Ghost
Gidi na Ghost
Image: RADIO JAMBO

Diana Ogallo ,27,  alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mume wake Collins Masanga ,26, ambaye walikosana naye takriban mwaka mmoja uliopita.

Diana alisema ndoa yao ya miaka minne baada yake kutofautiana na mumewe kuhusu masuala madogo madogo.

"Mama yangu alikuwa mgonjwa vibaya akalazwa. Nikapigiwa simu nikaambiwa niende nikae na yeye. Kurudi mume wangu akaniambia niende nikae na mamangu. Nikarudi kwa mama yangu akawa mgonjwa tena nikampeleka hospitali. Bwanangu alisema niendelee kukaa na mamangu juu ananipenda," Diana alisema.

Diana alisema hawakuwa wamepata mtoto kwa kuwa mumewe alikuwa amependekeza wajipange kwanza kabla ya kuwa wazazi.

Ghost alipopiga simu ya Collins aliyechukua ni mwanadada ambaye alidai kuwa ni mke wake. Sekunde chache baadae hata hivyo Collins alichukua sumu na kueleza sababu zake kutengana na Diana.

"Nilimwambia nilikuwa na bibi kabla nijitose kwenye mahusiano naye. Sikumblacklist kwa kupenda, vile huyo mwanadada alikuja ikawa shida nikaona nimblacklist niokoe ndoa yake. Ata nilikuwa na mtoto naye. Ni mtoto wangu," Collins alisema.

Alidai kuwa mahusiano yake na Diana yalifika kikomo takriban miaka miwili iliyopita. Alimwagiza mpenzi huyo wake wa zamani asonge mbele na maisha yake kwani yeye tayari yupo kwenye ndoa nyingine.

"Ni miaka miwili imepita tangu tukatize mahusiano. Haiwezekani. Tayari mimi nishamove on. Kile ambacho anaweza kufanya ni kumove on. Nakutakia maisha mazuri. Shusha moyo wako na utaweza kupata mwingine. Hutaweza kusonga mbele ukiwa na chuki," Collins alimwambia Diana.

Diana ambaye alisikika kughadhabishwa na maneno hayo alidai Collins kuwa hakuwahi kumwambia kuwa ana mpenzi mwingine ambaye alipata mtoto naye.

"Hakuwa ameniambia eti ako na mwingine. Endelea kuishi maisha yako. Endelea kulea mtoto wako. Kuja uchukue nguo ulizoninunulia upatie huyo mwenye mko naye" Alisema.