"Aliniambia nimsahau!" Mwanadada asimulia jinsi alivyodhalilishwa na mpenzi wa mumewe

Muhtasari

•Newton alisema mkewe aligura ndoa yao ya miaka miwili takriban miezi sita iliyopita baada ya kumshuku kuwa ana mke mwingine.

•Purity alifichua kuwa kuna mwanadada ambaye alimwarifu kuwa ni mpenzi wa mumewe na hata wana mtoto pamoja.

Gidi na Ghost
Gidi na Ghost
Image: RADIO JAMBO

Katika kitengo cha Patanisho, Jamaa aliyejitambulisha kama Newton aliomba kupatanishwa na mke wake Purity Gakii.

Newton alisema mkewe aligura ndoa yao ya miaka miwili takriban miezi sita iliyopita baada ya kumshuku kuwa ana mke mwingine.

“Mimi ni dereva. Nilipata kazi ya malori nje . Baadae bibi yangu akanipigia simu akidai huwa siwapigii simu na kutuma pesa. Alisema niko na bibi mwingine nje ndio maana huwa sipigi simu. Nilikuwa tayari kumbeba ndio ili athibitishe kuwa sina," Newton alisema.

"Nilipigiwa simu na mamangu akaniambia kuwa  bibi yangu alienda. Aliacha kama amesema kuwa aliolewa na mtu wala sio nyumba," Aliongeza.

Jamaa huyo alipuuzilia mbali madai ya kuwa na mke mwingine na kujijihusisha na mipango ya kando. Alisema kwamba sasa anahangaika sana nyumbani kwa kuwa mkewe hayupo kusaidia.

Purity alipopigiwa alidai kuwa uhusiano na mawasiliano yake na mumewe yalibadilika wakati alipoenda  kazi mbali

Aidha alifichua kuwa kuna mwanadada ambaye aliwahi kupokea simu ya mumewe na kudai kuwa ni mke wake.

"Ni kweli alienda kazi nje na hata huwa hapigi simu na niko na mtoto mdogo. Alikuwa ameacha pesa kidogo tu. Nikimpigia simu alikuwa anaongea kidogo alafu anakata. Siku ingine nilimpigia simu ikachukuliwa na mwanamke mwingine ambaye  alianza kunitusi," Alisema.

Newton alikana kuwa mwanadada huyo alikuwa mpenzi wake huku akidai kuwa ni mhudumu katika hoteli aliyokuwa analala.  

“Kuna mwanadada alishika simu yangu nilipoiacha  kwa moto. Baadae nilipochukua simu nikapata mke wangu alikuwa amepiga simu. Nilimuuliza alichomwambia akasema alimwambia kuwa siko karibu," Alisema.

Purity hata hivyo alifichua kuwa mwanadada huyo alimwarifu kuwa ni mpenzi wa mumewe na hata wana mtoto pamoja.

"Nilimuuliza Newton ako wapi akaniambia kuwa yeye ndiyo ako na simu. Alisema yeye ni mke wake na hata wana mtoto pamoja. Aliniambia nimsahau basi kwa sababu ni bwana yake.  Mimi nilikasirik nikakata simu," Alisema.

Baada ya kukana kwa muda hatimaye Newton alikiri kuwa alitoka kimapenzi na mwanadada mwingine alipokuwa kazini.

Purity hata hivyo alisema yupo tayari kumsamehe ikiwa angechukua hatua ya kuenda kwao na wazazi wake.