Jamaa aachwa baada ya kuenda photoshoot na ex wake na kupakia picha WhatsApp

Alidai kuwa alikuwa amekutana na mpenzi huyo wake wa zamani kwa ajili ya kushiriki chakula pamoja.

Muhtasari

•Ibrahim alisema marafiki wa mpenziwe walichukua screenshot ya picha iliyopakiwa kwenye WhatsApp yake na kumtumia.

•"Nilijaribu kumpigia ex wake simu baada ya photoshoot akaniambia kuwa wanachumbiana," Chemutai alisema

Ghost Mulee na Gidi Ogidi
Ghost Mulee na Gidi Ogidi
Image: RADIO JAMBO

Ibrahim Orata ,22, alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mchumba wake Daisy Chemutai ,21, ambaye alimtema mapema mwaka huu.

Alieleza kuwa mpenziwe ambaye pia ni mwanafunzi mwenzake katika chuo kikuu alimuacha baada ya kipindi cha likizo.

"Vile tulienda likizo mimi nilienda kwetu naye  akaenda kwao. Nilikutana na ex wangu, mpenzi wangu alikuwa anamjua. Vile tulikutana tulipiga picha. Ex wangu alichukua simu akajipost kwa simu yangu," Ibrahim alisimulia.

Ibrahim alisema marafiki wa mpenziwe walichukua screenshot ya picha iliyopakiwa kwenye WhatsApp yake na kumtumia.

"Wakati huo mpenzi wangu hakuwa online. Marafiki wake waliscreenshot wakamtumia," Alisema.

Alidai kuwa alikuwa amekutana na mpenzi huyo wake wa zamani kwa ajili ya kushiriki chakula cha mchana pamoja.

Nilikuwa nimeongea na mpenzi wangu kuhusu mkutano wangu na ex na alikuwa amenisamehe. Lakini marafiki wake walieneza fitina na hapo akaniacha,"

Chemutai alibainisha kuwa ni ngumu sana kwake kumuamini tena Ibrahim. Alisema tayari alikuwa amemuonya dhidi ya kukutana na mpenzi huyo wake wa zamani ila akakaidi na wakaendelea kukutana.

"Ni ngumu kumsamehe kwa sasa. Siwezi kumuamini tena. Mimi nilimkataza kupatana na yeye. Walikuwa wameenda kwa photoshoot wakapiga picha na akaweka kwa status. Mimi sikuwa online," Alisema Chemutai.

Alisema aliamua kujitenga na mchumba huyo wake kwani hasira nyingi zilimpanda kila alipokumbuka yaliyojiri.

"Nilijaribu kumpigia ex wake simu baada ya photoshoot akaniambia kuwa wanachumbiana.. Yeye atie tu bidii na akipata msichana akuwe mwaminifu," Alisema.

Gidi alimshauri Ibrahim kumpatia mpenziwe muda na kutumia kipindi ambacho wametengana kujiangazia na kujirekebisha.