Patanisho: Mwanaume aliyetaka wanawake wawili, akataliwa na wote

Reagan alienda nje ya ndoa na mke wake Terry, akaoa mwanamke mwingine ambapo wote walipogundua walimwacha

Muhtasari

• Reagan alitaka kurudiana na Terry baada ya kuachana naye kwa mwaka mmoja alipoenda nje ya ndoa.

• "Nimeolewa nina mwanaume mwingine," Terry alisema.

Gidi
Image: Radio Jambo

Katika kipindi cha Gidi na Ghost asubuhi kitengo cha Patanisho, jamaa aliyejitambulisha kama Reagan alituma ujumbe akitaka kupatanishwa na mke wake Terry.

Reagan alisema kuwa alitengana na mke wake mwaka mmoja uliopita kwa kuwa alienda nje ya ndoa.

Alieleza kuwa walipatana na mkewe mjini wakachumbiana kwa muda kisha akampeleka nyumbani kwao, yeye akabaki mjini alipokuwa anafanya kazi na kuanza anasa za dunia.

"Nilipompeleka Terry nyumbani, nilirudi mjini ambapo nilipatana na msichana mwengine nikamuoa," Reagan alisema.

Alisema kuwa mambo hayakuwa mazuri kati yake na mwanamke wa pili kwani alikuwa anafahamu kuwa alikuwa kwenye ndoa na Terry.

Baadaye mwanadada huyo alianza kumcheza ndipo baadaye akaamua kumwacha.

Mke wa Reagan, Terry alipopigiwa alisema kuwa hataki kurudi kwenye uhusiano naye.

"Wacha akae na huyo mwanamke, ni kama alikuwa na maana kuniliko , mbona ana majuto sasa? Huenda anawadanganya kuwa ameachana na huyo mwanamke mwingine,"Ruth alisema.

Aliongeza kuwa angekuwa na uhakika kuwa mume wake aliachana na side chick huyo iwapo angepigia na kumwambia mwenyewe.

Tuliachana naye na nilikuwa nataka turudiane

"Wewe baki na huyo msichana, ulikuwa unampenda na uliniambia kuwa unampenda zaidi ya unavyonipenda mimi. Nimeolewa nina mwanaume mwingine," Terry alisema.

Mama huyo alisema kuwa mwanaume huyo mwingine ambaye wanachumbiana sai amekuwa akimtunza na kumwonyesha mapenzi hata kumkubali mwanawe.

"Huyu alikubali kuwa baba ya mtoto, wewe ulikataa, mimi sirudi,"alisema.

Zaidi ya hayo, Terry alieleza kuwa Reagan alikataa kumsaidia kulea mtoto wao ikabidi aanze kusaidiwa na wazazi wake mpaka pale alipopata mwanume mwingine.

Reagan alizidi kusisitiza warudiane kwani alikuwa amethibitisha kutoka kwa dada yake Terry kuwa bado hakuwa ameolewa.

"Reagan alikuwa ananipenda na hawezi amini naeza kufanya kitu kama hicho, yeye aoe huyo mwingine, hana msimamo usipomuumiza haezi ridhika," Terry alisema.

Hata hivyo Terry alikiri kuwa kuna uwezekano wa kumsamehe Reagan iwapo tu ataomba msamaha mbele ya wazazi wake.

"Nilikuwa nakupenda na bado nakupenda, sitawahi kucheza tena," Reagan alisema huk akiwa amefurahi," alisema.