Patanisho: Jamaa akosea namba ya mpenzi aliyetaka kupatanishwa naye na ya mpenzi mwingine

"Huyo ni Sylvia, nilikuwa nataka Irene. Kwani hiyo namba inaisha na?" Wepukhulu alihoji.

Muhtasari

•"Kuna msichana mwingine alinipigia simu. Kumbe alikuwa amedivert simu zangu. Nilijaribu kujitetea, ikashindakana," Wephukulu alisema.

•Gidi alipopiga namba ambayo Wephukulu alituma, mwanamke mwingine aliyejitambulisha kama Sylvia alishika.

Gidi na Ghost
Gidi na Ghost
Image: RADIO JAMBO

Caleb Wepukhulu ,29, kutoka Uganda alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mchumba wake Irene Nambuga ,23, ambaye alikosana naye mwaka uliopita.

Wepukhulu alisema mchumba huyo wake ambaye alikuwa amechumbiana naye kwa zaidi ya mwaka mmoja alimtema Aprili mwaka jana baada ya kugundua anawasiliana na mwanadada mwingine wa Murang'a kwa simu.

"Kuna msichana mwingine alinipigia simu. Kumbe alikuwa amedivert simu zangu. Nilijaribu kujitetea, ikashindakana," Wephukulu alisema.

Alisema tangu wakati huo, Irene amekuwa mkali kwake na amekuwa hawasiliani naye vizuri licha ya kumuomba msamaha.

"Ata akienda nyumbani hawezi kuniambia anaenda. Namuomba anisamehe, haskii. Amekuwa mgumu," alisema.

Wephukulu alidai kwamba tayari amekatiza uhusiano na mwanadada aliyemfanya kukosana na mchumba wake.

Gidi alipopiga namba ambayo Wephukulu alituma, mwanamke mwingine aliyejitambulisha kama Sylvia alishika.

Sylivia alifichua kwamba alikuwa mke  wa Wepukhulu kwa muda na kudai kwamba Mganda huyo ni tapeli wa mapenzi.

"Irene ni mwingine alikuwa na yeye. Mimi ni Sylvia. Nilikuwa naishi nayeye," Syliva alisema.

Aliongeza, "Huyo ni mkora. Juzi nilimpigia simu akapatia mrembo mwingine. Namjua huyo Irene, alikuwa anaongea na yeye kwa simu. Mimi nilikuwa mke wake nimetoka kwake hivi majuzi."

Baada ya Wepukhulu kugundua amekosea namba, alisema, "Huyo ni Sylvia, nilikuwa nataka Irene. Kwani hiyo namba inaisha na?"

Alikiri kuwa Sylvia alikuwa mke wake ila ndoa yao ikasambaratika kufuatia masuala mbalimbali yaliyowatenganisha.

Sylvia alimshauri mume huyo wake wa zamani amtafute Irene na wajenge ndoa naye.

"Caleb, mtafute Irene umove on na yeye. Biashara ya mapenzi sipendi. Usinitext na usinipigie simu. Uongo haisaidii," alisema.

Ingawa Caleb alikiri kuwa alimpenda Sylvia, alisema hana chochote cha kumwambia.