Patanisho: Mwanajeshi wa KDF ahuzunika baada ya mkewe kukataa kuishi naye Mombasa

Boniface alisema kwa sasa Betty amemblock kwenye simu na amekosa namna ya kuwasiliana naye.

Muhtasari

•Boniface alisema aizozana na Betty takriban wiki mbili zilizopita baada  ya kumuomba ahamie jijiniMombasaambako anaishi.

•Betty alipopigiwa simu alikata pindi tu baada ya kusikia ombi la patanisho lilitumwa na Boniface.

Ghost Mulee na Gidi Ogidi
Ghost Mulee na Gidi Ogidi
Image: RADIO JAMBO

Kwenye kitengo cha Patanisho, Boniface mwenye umri wa miaka 39 alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mke wake Betty.

Boniface ambaye ni afisa wa KDF alisema aizozana na Betty takriban wiki mbili zilizopita baada  ya kumuomba ahamie jijiniMombasaambako anaishi.

“Nilikuwa nataka Betty akuje Mombasa. Akawa na sababu mbalimbali. Mfano, alikuwa na kesi fulani ya FIDA. Akasema amalizane nayo kwanza,” alieleza.

Aliongeza, “Kuna Bwana mmoja alikuja akamzalisha mtoto na akakataa kumhudumia. Hiyo kesi iliahirishwa hadi mwaka huu. Nilimwambia kama ni suala kesi atakuwa anaenda Nairobi kufuatilia. Ilifika mahali tukagombana na kukosana. Kwa sasa hatuna maelewano.”

Boniface alisema kwa sasa Betty amemblock kwenye simu na amekosa namna ya kuwasiliana naye.

“Hiyo nyumba anaishi Nairobi nilikuwa nalipia. Kwao sijaenda, tulikuwa na mpango wa kuenda,” alisema.

Alisema walianza uhusiano wao mwaka wa 2017 ila bado hawajafanikiwa kupata mtoto kwa jinsi wanavyoishi mbali na mwingine.

“Kukosana imetokea tu suala la yeye kuja Mombasa na kesi yake. Nilimwambia hakuna haja ya kukaa mbali,”

Betty alipopigiwa simu alikata pindi tu baada ya kusikia ombi la patanisho lilitumwa na Boniface. Alikataa katakata kushika simu yake tena alipopigiwa na Gidi.

Kufuatia hayo, Boniface alisema, “Ni dhihirisho wazi kuwa amekata kauli.

Aidha alifichua kuwa sio mara ya kwanza kwa Betty kumblock huku akieleza kwamba mkewe ni mtu wa hasira.

“Yeye ni mtu mwenye hasira sana. Hiyo mambo ya kublock haijaanza leo. Huwa anafanya hivyo mara nyingi sana. Hii ya saa hii naona kama imekaa sana. Lakini kuna ile ilichukua miaka miwili,” alisema.

Alipopewa nafasi ya kuzungumza na Betty hewani alisema, “Nakuomba uniunblock kwa simu tuongee. Kama nimekukosea naomba unisamehe. Bado nakupenda.