Patanisho: Mume wangu alinipata na mtu, nilijaribu kumbembeleza akakataa

"Nilijaribu kumbembeleza kwa kumwekea mkono tukilala, lakini alikuwa anasusa kwa kuutupa mkono wangu kando", mwanamke alisema.

Muhtasari

• Mwanadada huyo wa miaka 21 alisema baada ya kufumaniwa, alijaribu kumwekea mumewe mkono lakini alikuwa anasusa kwa kuutupa kando.

• Mwanadada huyo ana miaka 21 huku mumewe akiwa na miaka 38.

Gidi na Ghost
Gidi na Ghost
Image: RADIO JAMBO

Mwanadada Vivian wa miaka 21 alipeleka malalamishi yake kwenye kitengo cha Patanisho kwa Gidi na Ghost akitaka kupatanishwa na mumewe, baada ya kutengana Desemba mwaka jana.

Mwanadada huyo alisema kuwa mumewe wa miaka 38 walikosana kidogo tu na akaamua kuondoka na kurudi kwao, katika kile alisema kuwa juhudi zote za kujaribu kumbembeleza mumewe ziligonga mwamba.

“Nilijaribu kumbembeleza lakini akakataa, nilijaribu kumwekea mkono wangu, anaurusha kando,” Vivian alisema.

Kwa upande wake mwanamume huyo kwa jina Abraham mweney miaka 38, alsiema kuwa hakumfukuza mkewe bali aliondoka nyumbani mwenyewe tu.

Abraham alisema alirudi nyumbani akamfumania Vivian kwenye boma lake wakiwa wameketi na mwanamume mwingine.

Alipomuuliza huyo mwanamume ni nani, Vivian alisema ni jirani yake lakini Abraham akapinga vikal ihilo akisema kuwa alikuwa anawajua majirani wake wote na huyo hakuwa mmoja wao.

“Mimi hufanya kazi Nairobi na huyu msichana nilimuoa niko na miaka 38. Nilimuacha kwa nyumba nikienda kazi, siku moja nikarudi kinyemela na nilimpata na mtu. Huyo msichana akatoroka akaenda na mtoto wangu mmoja,” Abraham alisema.

Vivian alipopewa nafasi ya kuzungumza na mumewe, alimtaka Abraham amfuate nyumbani kwao ili waweze kuyasuruhisha na kurudi, lakini Abraham hakuwa tayari kutekeleza wazo hilo nay eye alibaki na msimamo wake kuwa kwa vile hakumfukuza Vivian basi hafai kumwendea.

Alimtaka Vivian kurudi mwenyewe vile aliondoka kwani yuko tayari kumsamehe iwapo atarudi.

Baadhi ya mashabiki wa Radio Jambo waliotoa maoni yao wengi walisema kuwa tatizo kubwa kati ya wanandoa hao ni utofauti mkubwa baina ya miaka yao.

Walimtaka Abraham kutafuta mwanamke wa rika lake kwani mwanadada huyo wa miaka 21 bado ana utoto na ndio maana alikuwa bado hajatulia na kutosheka naye pekee.