Patanisho: Mwanaume amkana mwanadada aliyedai kuwa alimwambukiza ugonjwa

Christine alisema alikuwa na mimba ya Cleophas ambayo ilitolewa baada ya kugunduliwa mgonjwa.

Muhtasari

•Christine alisema alikuwa amepanga ndoa na Cleophas ila mipango  ikagonga mwamba baada ya mchumba huyo wake kugundua ni mgonjwa.

•Cleophas alisema kwamba Christine ambaye anamjua sio ambaye alikuwa anazungumza kwa simu.

GHOST NA GIDI STUDIONI
GHOST NA GIDI STUDIONI GHOST NA GIDI STUDIONI
Image: RADIO JAMBO

Christine ,30, kutoka Kisumu alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na aliyekuwa mchumba wake Cleophas ambaye alikosana naye mwaka jana.

Christine alisema alikuwa amepanga ndoa na Cleophas ila mipango  ikagonga mwamba baada ya mchumba huyo wake kugundua ni mgonjwa.

"Kabla nipatane na yeye nilikuwa nimeolewa kwingine na nikapata watoto wanne. Niliachana na huyo kwa sababu ya mambo ambayo siwezi kueleza. Alikuwa anapenda wanawake sana," Christine alisimulia.

Aliendelea, "Mwaka jana Disemba nilipatana na Cleophas. Ilikuwa tuoane mwaka huu. Kumbe nilikuwa mgonjwa na sikujua. Nilienda hospitali na nikapewa dawa." 

Christine alisema kwamba mchumba huyo wake ndiye aliyemuarifu kuhusu ugonjwa huo baada ya kufanyiwa vipimo hospitalini.

Aidha alifichua kwamba alikuwa na mimba ya Cleophas ambayo ilitolewa baada ya kugunduliwa kuwa na ugonjwa.

"Nilifanyiwa vipimo lakini nikaambiwa nyumba ya mtoto haiwezi kubeba ujauzito. Mimba ilitolewa alafu nikatibiwa," alisema.

"Wakati nilikuwa na yeye alipata dalili akaenda akajipima. Siwezi kujua kama mimi ndiye nilimwambukiza, alisema mimi ndio nilimpatia. Mimi nilikuwa najua niko sawa. Nilidhani kuna mtu nilikutana na yeye akanipatia ugonjwa.  Wiki jana nilienda hospitali nikajua ugonjwa iko. Ndio maana nikatolewa mimba."

Alisema kuwa tangu wakati huo Cleophas hajakuwa akishika simu zake wala kujibu jumbe zake.

Cleophas alipopigiwa simu alisema kwamba hamfahamu Christine dewe wala sikio.

"Wewe unanipeleka Radio Jambo na mimi sikujui. Mimi sikujui. Mimi sijawahi kupelekwa Radio Jambo kwa hivyo sikujui.  Hiyo sauti siifahamu. Mimi siwezi kubali mtu ambaye simjui. Mimi simjui," alisema.

Cleophas alisema kwamba Christine ambaye anamjua sio ambaye alikuwa anazungumza kwa simu.

Kufuatia hayo, Christine alimsihi mchumba huyo wake wa zamani atulize roho yake na akubali warudiane huku akimhakikishia kuwa bado anampenda.

"Sikujui na sikutambui. Hiyo upendo unasema siitambui. Labda unitafute nithibitishe ni  wewe," alisema.