Patanisho: Jamaa amzuia mpenziwe kuenda shule, ataka waoane kwanza

"Nakupenda. Wewe ndo wangu wa maisha," Naomi alimwambi Samuel.

Muhtasari

•Naomi alisema mchumba wake alikasirika baada ya kufahamu mipango yake ya kuendeleza masomo katika chuo kikuu.

•Samuel alisema kwamba hangeweza kuzungumza mengi kwa kuwa yupo kazini.

Ghost na Gidi
Ghost na Gidi
Image: RADIO JAMBO

Brilliant Naomi ,21, kutoka Voi alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mchumba wake Samuel Mudema ambaye alikosana naye hivi majuzi.

Naomi alisema mchumba wake alikasirika baada ya kufahamu mipango yake ya kuendeleza masomo katika chuo kikuu.

Kaka yangu alikuwa anataka kunirudisha shule. Sikuwa nimemueleza. Nilimueleza baadae," alisimulia Naomi.

Aliongeza, "Alikuwa anataka niende  shule lakini alitaka niende baadae. Alitaka tuoane kwanza."

Samuel alipopigiwa simu, Naomi alichukua fursa hiyo kumuomba msamaha mpenzi wake kwa hatua aliyochukua.

"Sawa, nimekusamehe," Samuel alisema.

Samuel alisema kwamba hangeweza kuzungumza mengi kwa kuwa yupo kazini.

Hata hivyo, alimtaka mpenzi huyo wake kusimamisha mipango ya kuenda shule na kusubiri waingie kwenye ndoa kwanza.

"Avumilie kidogo. Tutaongea na yeye baadaye," alisema.

Naomi alimshukuru mpenzi huyo wake kwa kukubali msamaha wake.

"Nakupenda. Wewe ndo wangu wa maisha," alisema.

Gidi hata hivyo alimshauri mwanadada huyo kuangazia masomo yake kwanza kwa kuzingatia kuwa umri wake bado ni mdogo. Alimtaka kutofanya maamuzi kwa kuzingatia mapenzi ila maisha yake ya usoni.