Patanisho: Kijana atumia mchungaji mwonaji kujua baba yake mzazi

Luka alisema amekuwa akipata ajali mara kwa mara baada ya kukosana na baba yake.

Muhtasari

•Luka alisema babake alimfukuza nyumbani baada ya majirani kumwambia kwamba alikuwa analeta wasichana nyumbani.

•Luka alitoa ombi kwa Bw Wekesa kumsamehe ili aweze kupata amani maishani.

GHOST NA GIDI STUDIONI
GHOST NA GIDI STUDIONI GHOST NA GIDI STUDIONI
Image: RADIO JAMBO

Luka alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na baba yake Peter Wekesa ambaye alidai alikosana naye kufuatia fitina za majirani.

Luka alisema babake alimfukuza nyumbani baada ya majirani kumwambia kwamba alikuwa analeta wasichana nyumbani.

"Nimelelewa na nyanya ambaye amezaa mama. Sikujua baba yangu ni nani. Siku moja nilienda kwa mchungaji muonaji nikaomba usaidizi wa kujua baba yangu. Mchungaji alitumia maono akanipeleka kwa boma yake," alisimulia.

Aliongeza, "Kufika pale nilipata baba mkubwa. Nilijitambulisha akaniambia niende nyumbani ataniunganisha na baba yangu.Tulijuana na baba mwaka wa 2018.  Aliniambia niishi kwa nyumba yake. Nilimwambia nataka kumtembelea nyumbani kwake Bungoma. Kukaa kidogo nikasema nirudi nyumbani."

Luka alidai kuwa ni baada ya kurejea nyumbani ndipo baadhi ya majirani walianza kupiga ripoti kwa baba yake wakisema kuwa analeta wanawake kwa nyumba, madai ambayo alikanusha na kueleza kuwa ni wanafamilia.

"Majirani walisema naleta wasichana. Baadae baba alinifukuza kwa nyumba akasema hataki mambo ambayo nafanya kwa nyumba. Sasa hivi napata ajali kila wakati. Ata juzi nimepata ajali," alisema.

Bw Wekesa alipopigiwa simu alisema, "Mwambie aende kwa wazazi kwenye wanaombeanga msamaha," kisha akakata simu mara moja.

Luka alisema amekuwa akijaribu juu chini kurejesha uhusiano wake na babake ila juhudi zake hazijazaa matunda.

"Huwa naenda mahali huwa anafanya kazi ananiacha hapo. Nimejaribu kutumia hata wanafamilia lakini amekataa.

Sijawahi kufanya kitendo kama hicho. Ni dada za mama yangu walikuwa wananitembelea. Alikuwa ameweka majirani kama wapelelezi," alisema.

Luka alidokeza kuwa ugomvi wake na babake huenda ulichangiwa na hali kuwa wazazi wake wawili walikuwa wametengana.

Hata hivyo, alitoa ombi kwa Bw Wekesa kumsamehe ili aweze kupata amani maishani.

"Mimi ata sitaki shamba, nataka tu amani kati yangu na wewe. Mahali nilipo sasa hivi nipate tu amani. Usiniache nikaangamia. Nimehepa ajali nyingi, Mungu ndiye ameniokoa," Luka almwambia baba yake.