Patanisho: Nampenda jinsi huwa napenda Busaa, nikikosa kunywa busaa sitafanya kitu

Sharon alifichua kuwa mpenzi huyo wake alikuwa anamtongoza dadake mdogo.

Muhtasari

•Wanyama alidai kuwa mpenziwe aligura ndoa yao ya miaka miwili baada yake kuenda kutafuta kazi bila kumuarifu.

•Sharon alipopigiwa simu alifichua kwamba mpenzi huyo wake alikuwa anamtongoza dadake mdogo.

Gidi na Ghost
Gidi na Ghost
Image: RADIO JAMBO

Jamaa kwa jina Samson Wanyama (23) kutoka Bungoma aliomba kupatanishwa na mpenzi wake Sharon Simiyu (20).

Wanyama alidai kuwa mpenziwe aligura ndoa yao ya miaka miwili baada yake kuenda kutafuta kazi bila kumuarifu.

"Nilikuwa nakaa tu kwa nyumba. Wiki iliyopita niliamua kuenda kutafuta kazi lakini sikumwambia. Nilitaka nikipata kazi nimpigie simu. Niliporudi nyumbani nilipata habari nyingi ati nilikuwa nimeoa bibi mwingine, lakini sio kweli," alisema.

Wanyama alidai kwamba baada ya mpenzi huyo wake kutoroka,mwanaume mwingine amekuwa akishika simu yake kila anapomigia.

"Aliniambia ako na mama yake atarudi baadaye. Kukaa bila bibi siku tatu ni kama mwezi mzima. Ilifanyika siku tatu zimepita. Hiyo siku tatu naona kama miaka tano," alisema.

Sharon alipopigiwa simu alifichua kwamba mpenzi huyo wake alikuwa anamtongoza dadake mdogo walipokuwa kwenye mahusiano.

"Wakati nilikuwa naishia nayeye. Alikuwa bado anaongea na dada yangu kama shemeji. Nikijaribu kumuuliza bado anaruka. Lakini nikiangalia mazungumzo yao yalikuwa ya kutiliwa shaka. Nilikuja kugundua anakatia dada yangu. Nikimuuliza alikuwa ananijibu  na madharau. Pia alikuwa na mipango ya kando," alisema.

Aliongeza, "Alikuwa anamtongoza dada yangu na akimuuliza kwa nini ilhali ako na mimi anasema mimi ni wa nyumba lakini yeye anampenda tu. Alikuwa anakatia Leah hadi kaka yangu akamuonya."

Sharon pia alifichua kwamba alimuarifu mpenzi huyo wake alipokuwa akiondoka na kumweleza sababu yake kuchukua hatua hiyo.

Wanyama hata hivyo alitupilia mbali madai ya kumtongoza dada ya mpenziwe.

Alipoulizwa kuhusu kulipa mahari alisema, "Wacha tuzae watoto kama watatu ndio nipeleke mahari."

Wanyama alimuomba msamaha mpenzi huyo wake na kumuahidi kurekebisha tabia zake .

"Kuanzia leo mambo na mipango ya kando nimeacha... Nampenda kama vile huwa napenda Busaa. Nikikosa kunywa hiyo sitafanya kitu," alisema.

Sharon alimwambia atume nauli ili aweze kurejea.