logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Gidi ajawa bashasha baada ya mwanafunzi wa Chuo Kikuu kuwasilisha utafiti kuhusu Patanisho

Mtangazaji Gidi amejivunia sana baada ya mwanafunzi wa CUEA kukamilisha tasnifu kuhusu kitengo cha Patanisho.

image
na SAMUEL MAINA

Vipindi05 May 2023 - 09:01

Muhtasari


  • •Songok Irvine Jepkoskei alifanya utafiti kuhusu nafasi ya redio katika kutatua migogoro ya kifamilia, mfano wa kipindi cha Patanisho.
  • •Gidi alibainisha kwamba hii sio mara ya kwanza kwa mwanafunzi kutumia ubunifu wake katika kazi kazi ya shule.
Ghost Mulee na Gidi Ogidi

Mtangazaji wa kipindi cha Gidi na Ghost asubuhi kwenye Radio Jambo Joseph Ogidi almaarufu Gidi amejivunia ubunifu wake baada ya mwanafunzi mmoja wa Chuo Kikuu cha Catholic University of East Africa (CUEA) kuwasilisha tasnifu yake kuhusu kitengo cha Patanisho.

Songok Irvine Jepkoskei alifanya utafiti kuhusu nafasi ya redio katika kutatua migogoro ya kifamilia, mfano wa kipindi cha Patanisho kwenye Radio Jambo n mbele ya jopo la wahadhiri.

Alikuwa ameratibiwa kuwasilisha tasnifu hiyo Ijumaa Mei, 5.

Huku akieleza furaha yake kuhusu hatua ya Irvine na kuipongeza, Gidi alimtakia kila la heri mwanafunzi huyo anapowasilisha kazi yake. 

"Leo hii, Irvine Jepksokei kutoka CUEA atakuwa akitetea pendekezo la tasnifu yake kutumia kitengo chetu cha radio Patanisho, tunamtakia kila la heri," Gidi alisema kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Instagram.

Mtangazaji huyo mahiri alibainisha kwamba hii sio mara ya kwanza kwa mwanafunzi kutumia ubunifu wake katika kazi kazi ya shule.

"Mwaka wa 2005, J Nyairo akiwa Afrika Kusini alitetea tasnifu yake ya PhD kutumia wimbo wetu Unbwogable. Tunamshukuru Mola kwa ubunifu," alisema.

Wakati wa kipindi cha Ijumaa asubuhi, Gidi alibainisha kuwa kitengo cha Patanisho kimeweza kutambuliwa sana kiasi cha kutumika katika masomo ya chuo kikuu. Alijivunia athari chanya ambayo imeletwa na kitengo hicho.

Patanisho ni moja ya vitengo katika kipindi cha Gidi na Ghost Asubuhi ambacho hupeperushwa kwenye stesheni ya Radio Jambo, Jumatatu hadi Ijumaa, kuanzia saa kumi na mbili asubuhi hadi saa nne asubuhi. Kitengo hicho ambacho hushabikiwa na mamilioni ya Wakenya na hata wengine nje ya nchi hupeperushwa mwendo wa saa mbili unusu asubuhi na wasikilizaji hupewa fursa ya kutoa maoni baada ya habari za saa tatu.

Lengo la kipindi cha Patanisho ni kuwasaidia waliokosana kusameheana na kurudiana, iwe wanandoa, wapenzi, wanafamilia, wafanyikazi wenza au watu wengine wale ambao wana uhusiano wa aina yoyote.

Usikose kusikiliza vipindi vya kusisimua vya Patanisho kila Jumatatu hadi Ijumaa, mwendo wa saa mbili unusu, vikiletwa kwako na watangazaji wako Gidi Ogidi na Jacob 'Ghost' Mulee.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved