Patanisho: "Hadi natokwa jasho!" Jamaa ashtushwa na mkewe kuomba wapatanishwe ilhali alidhani wako sawa

"Nauli haijakosa. Kuna mradi naendeleza huku. Sitaki kumwambia na hata sijawahi kumwambia," Abel alisema.

Muhtasari

•Esther alisema alihudhuria matanga nyumbani kwao mwishoni mwa mwaka jana na tangu wakati huo hajawahi kurudi kwa ndoa yake.

•Abel alikiri kwamba hatua ya mkewe kuomba kupatanishwa naye ilimshtua sana kwani alidhani mambo yao yapo shwari.

Gidi na Ghost
Gidi na Ghost
Image: RADIO JAMBO

Esther Nyaboke alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mume wake Abel Mukwa ambaye alitofautiana naye Desemba mwaka jana.

Esther alisema alihudhuria matanga nyumbani kwao mwishoni mwa mwaka jana na tangu wakati huo hajawahi kurudi kwa ndoa yake.

Tulikosana wakati nilitoka kwenda matanga nyumbani. Kutoka hapo ikawa ni kama tunabishana hadi wa leo. Huwa ananidanganya anatuma nauli lakini hatumi. Hataki kunitumia nauli. Nikimuuliza anasema hana," Esther alilalamika.

Esther alisistiza kuwa angependa kujua ikiwa mahusiano yao bado yapo imara ama mumewe alimtema bila kumuarifu.

Abel alipopigiwa simu alisema, "Bado tuko pamoja. Kuna vile maisha saa hii iko sio vizuri."

"Sijakucha. Si nimeongea na wewe jana jioni hadi leo jioni. Nitakujibu leo jioni. Ilikuwa ukuje Jumamosi, lakini kuna vile nilikuwa natarajia sijafaulu. Leo ndio natarajia mambo yatakuwa sawa," alimwambia mkewe.

Abel alikiri kwamba hatua ya mkewe kuomba kupatanishwa naye ilimshtua sana kwani alidhani mambo yao yapo shwari.

"Nimeshtuka hadi natoka jasho... Pesa inapatikana. Lakini kuna mradi tulikuwa tumepanga na yeye nashughulikia. Nauli haijakosa. Kuna mambo naendeleza huku. Sitaki kumwambia na hata sijawahi kumwambia," alisema.

Aliongeza, "Ilikuwa akuje Jumamosi lakini kuna vile nilichelewa kidogo nikamwambia kufikia leo jioni atapata nimemtumia nauli akuje kesho asubuhi."

Esther alikubali kumsuburi mumewe atume nauli na kumhakikishia kwamba nado anampenda sana licha ya yaliyotokea.

Katika jibu lake, Abel alimwambia, "Mimi nakupenda jinsi ulivyo. Nimekumiss sana. Nitakwambia mengi ukikuja huku mahali niko. Mi nampenda kama nyama. Anajua kwangu asipopika nyama ataenda asubuhi na mapema."