Patanisho: Jamaa apata kazi kwa kaunti na kumtoroka mkewe mjamzito wa mapacha

Wawili hao walikuwa kwenye uhusiano kwa mwaka mmoja na nusu na walipata mtoto wa kwanza akafariki na bahati nzuri mimba ya pili ikawa ya mapacha lakini mume akaingia mitini.

Muhtasari

• Mrembo huyo ambaye ni mjamzito wa miezi 7 alisema kuwa awali alipata mtoto wa kwanza na Ouma lakini kwa bahati mbaya mtoto akafariki.

• Mrembo alisema kuwa kwa kipindi chote wamekuwa pamoja, hakufanikiwa kujua kwa kina mumewe wala kujuana na watu wa kwao.

Ghost Mulee studioni
Ghost Mulee studioni
Image: RADIO JAMBO

Katika kipindi cha patanisho Ijumaa asubuhi kwenye Radio Jambo, mwanadada Yvonne Maureen mwenye umri wa miaka 30 kutoka Bondo kaunti ya Siaya alipeleka ombi akitaka kupatanishwa na mpenzi wake Joshua Ouma mweney umri wa miaka 35.

Kwa mujibu wa Maureen, wamekuwa kwenye uhusiano kwa mwaka mmoja unusu, ambao ni uchumba lakini walikosana mapema mwezi Mei baada ya Ouma kupata ujumbe kutoka kwa kaunti kuwa amepata kazi.

“Nilikosana na yeye tarehe nane huu mwezi baada ya yeye kupata kazi kisha akaamua kunyamaza. Kwa hivi sasa niko kwa Dada yangu Mkubwa maeneo ya Kisumu na yeye pia ako Kisumu lakini sijui pande gani,” Maureen alisema kwa sauti ya unyonge

Ouma alipopata kazi kwa kaunti, aliamua kunyamaza na Maureen ambaye ni mjamzito alisafiri kwenda Kisumu kwa dadangu na kipindi chote hicho Joshua hajawahi kumzungumzia.

“Dadangu alijaribu kumpigia simu akachukua na kusema kwamba yeye hana maneno mingi na mimi bali ni vocha tu huwa anakosa. Bado tuko tu kwa uchumba na hatujaoa. Tumekaa kwa mwaka mmoja na nusu,” Maureen alisema.

Mrembo huyo ambaye ni mjamzito wa miezi 7 alisema kuwa awali alipata mtoto wa kwanza na Ouma lakini kwa bahati mbaya mtoto akafariki na hii ni mimba ya pili ambayo ako nayo na anatarajia kupata mtoto wake mwezi Julai.

“Nilipata mtoto mwingine na Joshua lakini akafa, nina mimba ya pili naye na nilienda hospitalini nikaambiwa ni mapacha,” Maureen alisema.

Maureen alisema kuwa kwa kipindi cha mwaka mmoja na nusus ambacho wamekuwa kwenye mahusiano na Ouma, hakuwahi kujua kwao wala kujua watu wa kwao. Walikutana tu mjini na kuanza kuchumbiana.

Mtangazaji Ghost alijaribu kumpigia Ouma simu mara ya kwanza haikuchukuliwa na mara ya pili akapokea lakini akanyamaza kabla ya kukata.

Maureen alipewa nafasi ya kumpa maneno ya mwisho Ouma baada yake kukataa kupokea simu ya Radio Jambo.

“Joshua nakuambia mimi bado nakupenda tu sana hata kama umebadili mawazo yako, kuja tu unishughulikie na ushughulikie watoto wako, niliambiwa ni mapacha…. Mimi sijakataa ukiendelea na maisha yako lakini uje tu uniwajibikie,” alimsihi.