PATANISHO

Patanisho, Jamaa amcheza mkewe ,alia kuachwa

Hata kwa ndoto sitwahi kumwota anisahau kabisa

Muhtasari

•Kwa upande mwingine Elizabeth, ameweka wazi kwamba aliufanya uamuzi wa mwisho na hivyo amsahau huku akisistiza kwamba pia kwa ndoto amsahau.

•Tangu kuondoka kwa mkewe Simon alieleza namna unavyokumbwa na upweke tangu aliporejea nyumbani na kumpata tayari ameondoka.

Ghost na Gidi
Ghost na Gidi
Image: RADIO JAMBO

Katika kitengo cha patanisho, ndoa ya karibu miaka 12 yavunjika baada ya mwanaume kudaiwa kutelekeza majukumu ya familia yake na kuweka mpango wa kando na pesa mbele.

Simon, alalamika kuachwa na mkewe Elizabeth mapema Jumanne aliporejea kutoka kazini na kumpata hayuko nyumbani kama alivyomuacha.

Kulingana naye, alielea kuwa siku iliyotangulia alichelechelewa kufika nyumbani mapema kama ilivyokuwa ada yake kwa kuwa mafuta yaliishia gari lake.

“Gari langu lilizima kwa kuisha mafuta nikakaa kwa barabara kwa muda mrefu ,nikafika nyumbani sikula, nikapigia mama mkwe akaniongelesha vibaya.Nilipata mke wangu amelala hapo amenikasirikia. Ni kama alikasirika sana nilipofika nyumbani nikiwa nimechelewa", alisema.

Tangu kuondoka kwa mkewe Simon alieleza namna unavyokumbwa na upweke tangu aliporejea nyumbani na kumpata tayari ameondoka.

Kulingana na Elizabeth, ameeleza kuwa kupanga kutoka kwa Simon haukuwa mpango wa siku moja. Alieleza kuwa tayari alikuwa amechoka naye na hakuwa na jingine ila kuondoka huku akikiri kwamba ameondoka bila kurudi nyuma kutokana na tabia ya mumewe.

“Nilikuwambia nitachoka nawe na siku moja nitaondoka na utakuja kujitia kuondoka kwangu.” Ameeleza Elizabeth kwa njia ya simu.Aliendelea kueleza kuwa mumewe amemfanya kama mfanyakazi wake, kila siku akirejea nyumbani ni pesa anahesabu na kulala bila hata kuongea nawe.

“Hujui hadhi ya mke nyumbani wewe! Umenifanya kuwa mfanyi kazi wako, mimi naishi kama mjane ilhali nina bwana.” Aliendelea Bi Elizabeth.

Alikiri kwamba 2018 alimfumania na mpango wa kando na Simon akamwamuru aondoke, kilichochangia Elizabeth kuweka ahadi na mjomba wake kwamba akitoka hatawahi kurudi kwake tena.

Kulingana na Simon, amejutia makosa amekuwa akifanya na kuahidi kurekebisha iwapo mkewe atarudi huku akisema kwamba anampenda kama ugali kwa mboga aina ya saka.

Kwa upande mwingine Elizabeth, ameweka wazi kwamba aliufanya uamuzi wa mwisho na hivyo amsahau huku akisistiza kwamba pia kwa ndoto amsahau.

Ungemshauri vipi Simon?