KITENGO CHA PATANISHO

Patanisho: Jamaa amsingizia mkewe kuwa na mpango wa kando, alia kuachwa

Huyo waaah! Namaanisha kuwa huyo ni kisirani sana sitarudi huko - Trizah alikiri

Muhtasari

•Aliishi kunishuku kuwa mimi nina mpango wa kando na sikuwa nao. Huko sirudi!

GHOST NA GIDI STUDIONI
GHOST NA GIDI STUDIONI GHOST NA GIDI STUDIONI
Image: RADIO JAMBO

PATANISHO: Katika kitengo cha patanisho, Kevin Igunzu ameomba kupatanishwa na mkewe Trizah Mukabi, baada ya kuwa kwenye ndoa kwa miaka miwili.

Kevin,27, anakiri kuwa walikosana na mkewe Januari 2023 alipoanza kushuku kuwa Trizah ana macho ya nje ambapo waliachana na mkewe akaenda kwao, lakini alipofanya uchunguzi wake wa kina alibaini kuwa huo ulikuwa uvumi tu hapakuwa na ukweli.

Ameeleza kuwa hawajawahi kukosana ila kilichochangia mzozo baina yao ni kuwa Trizah alianza kubadilika kwa kwa nyumba na hatimaye akenda kwao Kiminini.

“Bibi yangu alifika pahali akabadilika kwa nyumba, nikamshuku alikuwa na mpango wa kando. Nilimwongelesha anajibu vile anataka, na mimi sikumkosea na hiyo ndiyo ilifanya akaenda kwao, na mimi siko tayari kuoa bibi mwingine, bado nampenda sana, huwa tu tunaongea kwa simu. Nilikuwa najipanga kwenda kwao. Nilikuwa najiandaa kumlipia mahari. Niliwahi enda kwao lakini nilisimama kwa barabara . Nilisimamam karibu na yao. Nilimpigia simu aklasema anarudi na sioni akirudi, nilikuwa nataka kujua msimamo wake, nijue kama anarudi au anaamuaje,” Alisimulia Kevin.

Kwa upande wake Trizah Mukabi, 22, aliapa kamwe hatarudi kwa mpenzi wake kwa sababu ya kutoaminiana. Ameeleza kuwa aliishi kumshuku kuwa ana mpango wa kando jambo lililomghadhabisha sana na kuamua kuachana naye.

Eti nikusamehe, na mbona ulifanya hivyo? Huko sirudi. Siwezi rudi huko. Ulidsanganya nilikuwa na mpango wa kando na sikuwa nao. Ilikuwa ni mazoea ya kila siku. Nimepata kazi lakini bwana bdo na simtaki. Huyo waah! Namaanisha kuwa huyo ni kisirani sana sitawahi rudiana naye,” Trizah alisimulia kwa njia ya simu.

Kevin, alieleza namna anavyompenda japokuwa mwanadada alishikilia msimamo wake kuwa hatarudi; “ haki mimi nampenda sana na sitaki kwenda kwa mwingine, Trizah haki mke wangu mimi bado nakupenda lakini kama hivyo ndivyo umeamua ni sawa,” Kevin aliendelea. Ungewashauri vipi wapenzi hawa wawili?