Patanisho: Jamaa ampa mimba mkewe hotelini, mtoto afikisha miezi 6 kama hajawahi kumuona

Kirui alikiri kwamba mwaka moja umepita tangu alipoonana na mkewe mara ya mwisho.

Muhtasari

•Kirui alisema ingawa hawajatengana, mkewe hajaweza kutulia nyumbani kwao kwani amekuwa anatoroka na kurudi kwao.

•Mama Chela aliweka wazi kuwa  mumewe kutoshughulikia mahitaji ya mtoto na kuwa na urafiki na wanawake wengi ndio mambo ambayo yamesababisha migogoro katika ndoa yao.

Image: RADIO JAMBO

Katika kitengo cha Patanisho, Jamaa aliyejitambulisha kama Aaron Kirui ,31, kutoka Nakuru alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mke wake Mama Chela ,26, kufuatia msukasuko kwenye ndoa yao ya miaka sita.

Kirui alisema ingawa hawajatengana, mkewe hajaweza kutulia nyumbani kwao kwani amekuwa anatoroka na kurudi kwao.

"Tumekuwa kwa ndoa kutoka 2017,  tulikuwa tukiishi na yeye kisha tukatoka tukaenda nyumbani. Baada ya miezi mitatu alitoka akaenda kwao. Alikaa kwao mwaka moja nikamwambia arudi. Akakaa miezi miwili alafu akatoroka tena. Alipoenda nilimuuliza shida ni nini akasema hata sijaenda kwao," Kirui alisimulia.

Aliongeza, "Tuko na watoto wawili. Alienda akarudi. Vile alienda akarudi  mara ya mwisho alikaa nyumbani wiki moja. Alikuwa mjamzito. Alienda akajifungua hospitali. Mimba ilikuwa yangu. Alipotoka hospitali alienda nyumbani kwao.  Nilimtumia nauli afike nyumbani kwetu akaniweka blacklist, baadaye asubuhi aliniambia atakuja. Saa hii sijui kama ako kwao ama ameoleka."

Kirui alikiri kwamba mwaka moja umepita tangu alipoonana na mkewe mara ya mwisho.

"Ako na karibu miezi sita tangu kutoka nyumbani. Tuko na karibu mwaka moja hatujaonana . Hiyo mimba alipata tukiwa Nakuru. Ilikuwa kwa hoteli ndogo," alisema.

Mama Chela alipopigiwa simu aliweka wazi kuwa  mumewe kutoshughulikia mahitaji ya mtoto na kuwa na urafiki na wanawake wengi ndio mambo ambayo yamesababisha migogoro katika ndoa yao.

"Yeye ndiye ako na shida, sio mimi. Angerekebisha hizo makosa ndogo ndogo, mimi sina shida. Ako na marafiki wengi, ukimueleza hataki kusikia. Nikitaka anitumie mahitaji ya mtoto mdogo anasema hana pesa, na ako kazi. Mtoto ako na miezi sita lakini hatumi pesa. Mtoto mkubwa ndiye alikatalia kwao," Mama Chela alisema.

Aliongeza, "Wakati nikienda kazi anafikiria mambo yake. Akirekebisha makosa yake mimi sina shida na yeye..Hajawahi hata kuona mtoto, ni mweupe ama ni mweusi. Si  hata angemwambia mama akuje asalimie mtoto."

Kirui alimuomba msamaha mkewe kwa makosa yake na kuahidi kuwa atarekebisha.

"Mama Chela mimi bado nakutambua kama mke wangu. Siwezi kurudi nyuma nitafuta mwingine. Kama ni hayio makosa nitarekebisgha," Kirui alimwambia mkewe.

Mama Chela alimwambia, "Akirekebisha makosa yake mimi sina shida na yeye."