Evans Odhiambo Oluoch kutoka kaunti ya Siaya alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mama mkwewe Pamela Auma ambaye alikosana naye kuhusiana na binti yake ambaye alikuwa kwenye mahusiano naye.
Evans alisema alikosana na mama mkwewe wakati alipotoroka kazini na kumuacha msichana wake baada ya kuzozana.
"Nilikuwa na msichana wake mwaka wa 2020. Nilienda kazi naye huko Seme. Hata sikumaliza kazi. Alikuwa ananipea masharti kwa sababu kaka yake ndiye alikuwa amenitafutia kazi," Evans alisimulia
Aliongeza, "Hata mtoto akilia alikuwa ananiambia niende nimshike. Nikisema kitu anasema nisiongee kwa sababu kaka yake ndiye amenileta hapo.Siku moja nilimwambia yeye anaweza baki mimi nirudi kwetu.Aliniambia ata nakaa mbwa siwezi kaa na yeye. Niliambia mdosi anisaidie na pesa ya chakula akanitumia. Nilitumia zile pesa nikamuacha mke wangu huko nikarudi nyumbani."
Alisema alizozana na mama mkwewe wakati alipojaribu kuwasiliana naye ili aweze kujenga na msichana wake.
"Nilipigia msichana 2021 ikiisha ili niweze kujenga nyumba na yeye. Niliona hachukui. Tuliongea na huyo mama ili nimuombe msamaha niwezi kusaidia mtoto kwa sababu msichana aliniambia hata akimwaga sukari anapigwa na huyo baba wako naye. Msichana hunipigia wakati mwingine. Ningeomba aniruhusu nikae na mtoto," alisema.
Aliendelea, "Alisema nilitukana msichana wake ati amekonda akaniambia nitafute msichana mnono tujenge naye."
Bi Pamela alipopigiwa simu alimzomea Evans na kufunguka kuhusu masaibu ambayo alimfanyia msichana wake
"Alichukua msichana. Hakuwa amekuja nyumbani. Walipofika huko kazi ikawa ngumu alirudi akaacha msichana huko. Kuna wakati alinitafuta eti alikuwa anataka kutuma transport msichana arudi. Nilimuambia juu alisema mtoto wangu ni mkonde atafute yule mnono. Nilimwambia aliacha msichana kwa stage watu wa bodaboda wamechukua," Bi Pamela alisema.
Evans hata hivyo alikiri makosa yake na kuomba msamaha .
Alisema aliyekuwa mpenzi wake huwa anampigia simu wakati mwingine na kumwambia shida ambayo wanapitia katika ndoa yake ya sasa.
Bi Pamela alimwambia, "Hujanikosea, kwa nini unaniomba msamaha? Vile nimeona, mpaka uko na shida ya kichwa, wewe ni mwenda wazimu. Hujawahi hata kusaidia mtoto. Unaomba mimi msamaha unaniombea nini?"
Aliendelea, "Mwenye ataleta mahari ndiye nitatambua kama bwana wa mtoto wangu.Uliza Evans msichana ako wapi. Mahali imefika, ninataka msichana kupitia kwake. Kama sio hivyo nitamshika kwa polisi."
Evans alisema, "Mimi bado nawapenda wote. Nitamtafuta msichana alafu nitamrudisha."
Mwishoni, Bi Pamela alimtaka Evans kumtumia shilingi elfu moja kama ishara ya kuomba msamaha.
Je, ushauri wako ni upi?