Patanisho: Mke mwenye hasira amfukuza mpango wa kando wa mumewe baada ya kuletwa nyumbani

"Alipoenda nilikuja na mwanamke mwingine kwa nyumba, akaambiwa kisha akakuja na akamfukuza," Wainaina alisimulia.

Muhtasari

•Wainaina alisema ndoa yake ya miaka saba ilivunjika Januari 2021 baada ya mkewe kuchoka na tabia yake ya ulevi na mipango ya kando.

•Wainaina alifichua kwamba licha ya kukosana na mkewe huwa anatembea kwao na hata kulala huko wakati mwingine.

Ghost na Gidi
Ghost na Gidi
Image: RADIO JAMBO

Katika kitengo cha Patanisho, jamaa aliyejitambulisha kama Dickson Wainaina ,33, kutoka Nyahururu alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mke wake Mary Wanja ,30, ambaye alikosana naye zaidi ya miaka miwili iliyopita.

Wainaina alisema ndoa yake ya miaka saba ilivunjika Januari 2021 baada ya mkewe kuchoka na tabia yake ya ulevi na mipango ya kando.

"Tulioana naye 2014 alafu nikaanza kunywa pombe sana baada ya kitu miaka tano hivi. Kuna wakati alinishika na mwanamke akanisamehe. Lakini sikuskia. Nilikuwa nakunywa pombe akachoka akaenda," Wainaina alisimulia.

Aliongeza, "Alipoenda nilikuja na mwanamke mwingine kwa nyumba, akaambiwa kisha akakuja na akamfukuza. Huwa tunaongea na yeye vizuri lakini ikifika ni kurudi anasema nimpatie muda. Alienda mara ya mwisho mapema mwaka jana." 

Wainaina alifichua kwamba licha ya kukosana na mkewe huwa anatembea kwao na hata kulala huko wakati mwingine.

"Najuta sana. Ako na watoto wetu wawili. Huwa nawasaidia," alisema.

Wanja alipopigiwa simu aliweka wazi kwamba hayuko katika nafasi ya kuzungumza na akakata simu mara moja.

"Sina nafasi ya kuongea. Mwambie nitamuongelesha," alisema Wanja.

Wainaina alifunguka kuhusu njia tofauti ambazo amejaribu kupatana na mkewe bila mafanikio ikiwemo kuwahusisha wazazi.

Alipopewa fursa ya kunena na mkewe hewani, alimwambia, "Mimi nakupenda. Maisha ni ngumu bila wewe. Tafadhali rudi kwangu tulee watoto wetu. Nakupenda."