"Mimba ni ya mwalimu, sio yangu!" Jamaa airuka waziwazi mimba ya mkewe ya miezi 8

"Mimi niko na shughuli zangu. Hiyo mimba ni ya huyo mwalimu, sio yangu. Sina stori yake huyo!" Elias alisema.

Muhtasari

•Elias aliendelea kumshtumu mkewe kwa kuwa na mahusiano na mwanaume mwingine ambaye alikuwa mwalimu wake katika shule ya upili'.

•Eznah alisema, "Mimi bado nampenda. Arudi tu tulee mtoto, mtoto ni wake aachane na maneno mingi."

Ghost na Gidi
Ghost na Gidi
Image: RADIO JAMBO

Katika kitengo cha Patanisho, mwanadada aliyejitambulisha kama Eznah Ingesu (21) kutoka Kisii alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mume wake Elias Amose (24) ambaye alikosana naye mwezi Agosti mwaka huu.

Eznah alisema ndoa yao ya miaka 2 ilisambaratika wakati mumewe alipomuacha kijijini kisha akaitiwa kazi na shangazi yake.

"Mume wangu alikuwa ameniacha ushago akaenda Nairobi., Shangazi yangu akanitafutia kazi mjini, kazi ya duka. Nikaamka nikaambia mamake kwamba shangazi yangu amenitafutia kazi mjini. Akasema ni sawa. Sikuwa na simu," Eznah alisimulia.

Aliendelea, "Alianza kupiga simu na kutusi shangazi yangu akisema niko kwa bwana mwingine. Nilitoka nikarudi nyumbani. Nikimpigia simu hataki kuongea na mimi. Nataka kurudiana naye juu niko na mimba ya miezi minane... Nilikuwa nimeambia shangazi yangu natafuta kazi juu niko na mimba na singeweza kutegemea mtu ako Nairobi na hatumi pesa. Sijui mbona anashuku nilienda kwa bwana mwingine. Yeye hakuwa anataka niende kazi. Alikuwa anataka nikae nyumbani lakini hashughulii mahitaji."

Elias alipopigiwa simu alitaka kujua mpenzi huyo wake yuko wapi huku akieleza kwamba hajui kabisa mahali aliko.

Alisema kuwa Eznah hakumwambia akienda kazi na hata alipompigia mama mkwe alisema hajui mahali aliko.

"Hakuniambia akienda, nilishtukia tu ametoka nyumbani akaenda. Mamangu alinipigia simu akaniambia Eznah ameenda. Nilichukua simu nikapigia mamake akaniambia hajui mahali ako. Mamake alimtafuta kwa jamaa zake wote," Elias alisema.

Aliendelea, "Wiki ijayo alirudi kwetu kitu saa moja asubuhi. Mama yangu alinipigia simu akaniambia kwamba Eznah amerudi. Nilimwambia aende kwao nitaenda tuongee hayo mambo. Saa hii sijui ako wapi."

Eznah alieleza,"Alipiga kelele mpaka hiyo kazi ikaleta shida. Alininyima pesa ya clinic akaniambia kama nataka niende kwetu. Ndio baba yake alinipatia pesa nikaenda clinic. Alituma 500 siku moja." 

Elias aliendelea kumshtumu mkewe kwa kuwa na mahusiano na mwanaume mwingine ambaye alikuwa mwalimu wake katika shule ya upili'.

"Kuna mwalimu naskia alimuoa hiyo wiki moja. Ni mwalimu alimfunza highschool. Walikuwa na mahusiano kwanzia akiwa form two. Wakati nilimpata alikuwa na huyo mwalimu. Nilimpata nikampeleka nyumbani. Kumbe bado walikuwa pamoja, mimi sikujua. Yeye mwenyewe aliniambia kuhusu huyo mwalimu. Nilipata wakichat"

"Huyo madam alimwitia kazi ni mwalimu. Ni shangazi yake lakini alikuwa amemwajiri kulea mtoto. Bwana ya huyo madam, alikuwa na uhusiano na Eznah. Ni hadithi kubwa. Huyu madam alimuita, mara ya kwanza alimwajiri kama kijakazi, Eznah alikuwa na uhusiano na bwanake," Elias alisema.

Eznah hata hivyo alitupilia mbali tetesi za mpenzi huyo wake na kusema, "Hapana, sikuwa na mahusiano na yeye. Nilipata mimba nikiwa Nairobi, nilikuwa nataka kuenda majuu akasema anataka nimuachie mtoto."

Elias pia alidai kuwa yeye sio mhusika katika mimba ya Eznah ila ni mwalimu ambaye alidai alikuwa na mahusiano naye.

"Sina stori na yeye. Acha ashughulikie huyo mwalimu. Mimi niko na shughuli  zangu. Hiyo mimba ni ya huyo mwalimu, sio yangu. Sina stori yake huyo. Ata yeye mwenyewe aliniambia ako na mwanaume atashughulikia hiyo mimba. Namuombea mazuri kwa huyo mwalimu. Waishi maisha marefu, Mungu awabariki," alisema.

Eznah alisema, "Mimi bado nampenda. Arudi tu tulee mtoto, mtoto ni wake aachane na maneno mingi."

Je, una ushauri gani kwa wawili hao?