Patanisho: Kijana ajuta baada ya kutumia 20,000 alizomwibia nyanyake kuwatumbuiza marafiki zake

Grivin alikiri kujuta uovu wake na kumuomba nyanya yake amsamehe na amsaidie kurudi shule.

Muhtasari

•Grivin alisema uhusiano wake na nyanyake uliharibika mwaka wa 2019 wakati alipumuibia zaidi ya shilingi elfu ishirini.

•Wakati huo nilikuwa mdogo, hakuna kitu ya maana nilifanya, niliwaspoil wenzangu tu." Grivin alisema.

Image: RADIO JAMBO

Jamaa aliyejitambulisha kama Grivin Nyongesa Baraza ,21, kutoka Bungoma alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na nyanya yake Pauline Wanyonyi ,68, ambaye alikosana naye takriban miaka minne iliyopita.

Grivin alisema uhusiano wake na nyanyake uliharibika mwaka wa 2019 wakati alipumuibia zaidi ya shilingi elfu ishirini.

Alijitetea kwa kusema hajui kilichomuingia akili akafanya kitendo hicho ila akabainisha kwamba anajuta sana.

"Mwaka wa 2019, nilikuwa katika kidato cha tatu. Kuna kitu iliingia akili, sikujua ni vibaya kumuibia nyanya yangu. Niliiba zaidi ya 20,000. Alikuwa ameweka kwa kabati tu lakini nilikuwa najua funguo zake," Grivin alisimulia.

Aliongeza, "Nyanya alliita kamati ya familia tukasuluhisha lakini naona bado hayuko sawa na mimi. Wakati huo nilikuwa mdogo, hakuna kitu ya maana nilifanya, niliwaspoil wenzangu tu."

Grivin alikiri kuwa nyanya yake ndiye aliyemsomesha hadi kidato cha nne na akabainisha kuwa kitendo chake kimefanya asiishi na amani.

Alisema angependa kumuomba msamaha nyanya yake na kumuomba ampe fursa nyingine na kumpeleka katika chuo kikuu.

Bi Pauline alipopigiwa simu, Grivin alichukua fursa hiyo kumuomba msamaha,

"Kuna wakati nilikuwa nimeiba pesa zako. Nilikuwa nataka unisamehe kabisa," Grivin alimwambia nyanyake.

Bi Pauline alimwambia, "Mbona tuko na wewe kwa boma na huwezi kusema, unaenda kwa radio? Tuko na wewe kwa boma, mbona uende kutangaza kwa dunia uonekane kama mwizi. Wewe mwenyewe ndiye uliaibika ukaondoka lna mimi nilitaka usome. Nilitaka uendelee na masomo ukaambiwa uende kazi. Mimi nilikushauri usome kwanza ukakataa ukaenda. Vile ulienda hukurudi na chochote."

Kuhusu kumsamehe mjukuu huyo wake, Bi Pauline alimwambia Ghost,"Hiyo siwezi kujibu wewe. Nataka aombe msamaha tukiwa kama familia."

Grivin alikiri kujuta uovu wake na kumuomba nyanya yake amsamehe na amsaidie kurudi shule.

Je, ushauri wako kwa Grivin ni upi?