Jamaa aliyemfukuza mkewe atia chumvi kwenye kidonda chake kwa kumleta Patanisho

"Anirudishie simu yangu, memory na battery. Kwanza nikikumbuka nililala kwa sakafu na hiyo baridi, achaa iishie hapo. Sitaki!!" Sheila alisema.

Muhtasari

•Bernard alisema alipata jumbe za kutiliwa shaka kwenye simu ya mkewe, jambo ambalo lilimpandisha mori hadi kufikia kumfukuza.

•"Hata akinipoteza, kwani ni mimi pekee kwa hii dunia? Hii ni maajabu! Nilimwambia tukutane nyumbani..," Sheila alisema.

GHOST NA GIDI STUDIONI
GHOST NA GIDI STUDIONI GHOST NA GIDI STUDIONI
Image: RADIO JAMBO

Bernard Mombo ,26, kutoka Nakuru alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mke wake Sheila Madokho ,23, ambaye alikosana naye takriban miezi sita iliyopita.

Bernard alisema ndoa yake ya chini ya mwaka mmoja ilisambaratika Mei mwaka huu wakati alipomfukuza mkewe baada ya kumshuku kuwa ana mipango wa kando.

Alisema alipata jumbe za kutiliwa shaka kwenye simu ya mkewe, jambo lililompandisha mori hadi kufikia kumfukuza.

"Nilikuwa nimeenda kazi mjini Nakuru nikaacha bibi nyumbani. Nilikaa mwezi mmoja. Wazazi wangu wakaanza kunipigia simu wakiniambia bibi yangu anaanza kubadilika, nikawaambia wampatie muda," Bernard alisimulia.

Aliendelea, "Niliporudi nyumbani mwezi wa sita, bibi akasema amekaa sana bila kuwaona wazazi wake. Nilishangaa kwa nini anataka kuenda wakati tu nimerudi, lakini nikamwambia aende tu, nilimpanga akaenda.  Akiwa kwao akaanza kunitumia jumbe akisema hajui huko kwetu kunakaa aje.  Nikamwambia aache maneno mingi arudi tuongee. Alikuja tukaongea na wazazi na tukasuluhisha. Baada ya wiki moja nikaona anachat kwa simu. Nikamuuliza ni kina nani anazungumza nao akasema nimuache. Nilimuomba simu yake nikapata anachat na wanaume, kumuuliza akasema ni marafiki wake. Juu ya hasira nikamwambia achukue vitu zake aende nyumbani kwao."

Bernard alisema hata hivyo baadae alifanya uchunguzi wake na kugundua kuwa ni kweli mkewe alikuwa anazungumza na marafiki zake.

"Nataka nimuombe msamaha kwa kuwa niligundua mimi ndiye mwenye makosa. Kwa kweli najuta," Bernard alisema.

Sheila alipopigiwa simu alidai kuwa tayari alikuwa amemueleza Bernard kuhusu msimamo wake ambapo alidai kila kitu ni sawa.

"Hiyo nayo ni noma. Sitaki kuongea. Tulichat na yeye. Tulisikizana, sasa ni nini anapeleka kwa redio?," Sheila alisema kabla ya kukata simu.

Bernard alisema imekuwa mazoea ya mkewe kusema atarudi ila hilo halikuji kutimia, "Anapenda tu kunienjoy, sasa nilitaka tu aniambie ukweli kama atarudi ama alimove on. Amezoea kusema atakuja, hiyo siku ikifika harudi. Nilitaka tu kujua ukweli kama atarudi. Mimi akiniambia harudi nitaangazia maisha yangu kwanza."

Sheila alipopigiwa simu kwa mara ya pili alisema, "Sitaki kuongea. Jana tuliongea nikamwambia mambo iko sawa. Kwa nini ananipeleka kwa redio, hata hiyo mambo naweza achana nayo. Namwambia mambo iko sawa alafu keshoye anakupeleka Radio Jambo?  Hata akinipoteza, kwani ni mimi pekee kwa hii dunia? Hii ni maajabu! Nilimwambia tukutane nyumbani.. Tutaongea baadaye. .

Huku Sheila akiendelea kufunguka kuhusu masaibu yake na Bernard, alisema hatua ya mpenzi wake huyo kuomba wapatanishwe imefufua kidonda ambacho alimsababishia moyoni wakati alipomfukuza.

"Anirudishie simu yangu, memory na battery. Kwanza nikikumbuka nililala kwa sakafu na hiyo baridi, achaa iishie hapo. Sitaki!!" alisema.

Bernard alimwambia, "Urudi juu nilikuwa nakupenda. Hakuna dame mwingine napenda."

Sheila alisema, "Sina maneno ya mwisho kwake."