Katika kipindi cha Gidi na Ghost asubuhi kwenye stesheni ya Radio Jambo, mwanamume kwa jina Shem kutoka Bungoma alitaka kupatanishwa na mpenzi wake Phyllis, ambaye alisema kwamba aliondoka na kwenda kwao mwaka jana kwa ahadi ya kurudi lakini hakuweza kurudi.
Shem alisema kwamba walikuwa wanaishi na mpenzi wake Nairobi wakati aliamka siku moja akisema kwamba alikuwa anaenda kumuona binamu wake Kapenguria.
Alipoondoka, hakuweza kurudi mpaka leo hii na Shem alisema kwamba kutoka wakati huo amekuwa akijaribu kumfuata mkewe lakini hachukui simu yake.
Shem alisema baadae alikuja anapatwa na ugonjwa uliomsababisha kuondoka Nairobi na kurudi nyumbani, lakini alisisitiza kwamba hakumkosea mkewe.
“Huyu mwanamke aliniambia binamu yake amemuita, halafu akaniambia anaenda na atarudi lakini kwenda huko akakwama nikimpigia simu hashiki… huo wakati tulikuwa Nairobi… ugonjwa ukanifikia sasa hivi niko nyumbani,” Shem alisema.
Phyllis aliopigiwa simu, alisema kwamba yeye alishasonga mbele na maisha yake wala hataki chochote na Shem.
Shem kwa sauti ya kuumia, alisema kwamba amekubali maji yameshamwagika na hayawezi kuzoleka. Kabla ya mrembo huyo kuenda kwao, Shem alikuwa ameishi naye kwa muda wa miaka 3 bila yeye kujitambulisha kwao.