Patanisho: Mwanadada aliyeugua baada ya kumuacha mpenziwe afurahi na kilio cha kuomba kusikika

Shantel alisema amekuwa akiugua na anahisi Joseph ni kila kitu kwake, sababu kubwa anahitaji msamaha wake.

Muhtasari

•Shantel alisema mahusiano yao ya miaka mitano yalisambaratika Machi mwaka jana baada ya yeye kumuacha Joseph na kuenda Saudia kwa ajili ya kazi.

•Alipopewa fursa ya kumwambia mpenziwe maneno ya mwisho, Shantel alisema "Hello my love.." kisha akaishiwa na maneno 

Ghost na Gidi
Ghost na Gidi
Image: RADIO JAMBO

Jumatatu asubuhi, mwanadada aliyejitambulisha kama Shantell Mbone (27)  kutoka Kakamega alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mchumba wake Joseph Lumire (32) ambaye alikosana naye mapema mwaka jana.

Shantel alisema mahusiano yao ya miaka mitano yalisambaratika Machi mwaka jana baada ya yeye kumuacha Joseph na kuenda Saudia kwa ajili ya kazi.

Alisema amekuwa akiugua na anahisi Joseph ni kila kitu kwake, sababu anahitaji msamaha wake. 

"Tulikosana kwa ajili ya makosa kidogo kidogo. Nikaamua kumove on nikaachana naye nikaenda kufanya kazi Saudi Arabia," Shantel alisema.

Aliongeza, "Kwa kuwa niko na shida ya cancer ilibidi nirudi mwaka huu mwezi wa saba. Naona siwezi nikamake pekee yangu. Tunaongea lakini naona bado ako na kinyongo ndani yake. Mimi ndiye nilikosea."

Shantel alifunguka wazi kuwa sababu ya kusimamisha mahusiano yao ni kwa kuwa Joseph alitaka atimize miaka 35 ndio waoane.

"Nimekuwa na huyo jamaa kwa miaka mitano. Nilifikiri tutaoana lakini alisema anataka afikishe miaka 35 ndiyo tuoane. Nikashangaa kama nitasubiri muda huo wote ndio tuoane nikaona nimove on. Aliniambia amenisamehe lakini nikiongea na yeye naskia bado ana kinyongo ndani ya roho yake," alisema.

Aliongeza, "Niliporudi nchini, binamu yangu aliniambia huyo jamaa alikuwa ananitafuta. Nikamtafuta nikamuomba anisamehe."

Joseph alipopigiwa simu aliweka wazi kuwa tayari amemsamehe mchumba huyo wake na hana kinyongo naye.

"Makosa iko lakini mimi nilisahau kila kitu. Nilimsamehe mimi siweki kinyongo. Nilikuwa nampea muda kwa sababu alikuwa anafanya kazi. Sikutaka kumtoa kwa kazi," Joseph alisema.

Aliongeza, "Mimi sioni makosa mahali. Kuna vitu mtu hufanya maishani ambayo ni reflection. Mimi sioni kama ulikisoa."

Shantel hata hivyo alimtaka mchumba wake kueleza kwa nini mapenzi ya awali hayapo tena. 

Joseph alijibu, "Unatarajia mtu atende kama awali? Lazima mtu achukue mapumziko.. nakupenda bado."

Kuskia hayo, Shantel kwa furaha alisema, "Mazee nashukuru sana. Leo niko na furaha.Nilikuwa na presha nyumbani. Hadi namuuliza utanizalisha lini mwanaume?"

Joseph alisema, "Mimi niko sawa. Hiyo ndio age niliona ni vizuri. Pia mimi sipendi mtu akiona kitu pia anataka."

Alipopewa fursa ya kumwambia mpenziwe maneno ya mwisho, Shantel alisema "Hello my love.." kisha akaishiwa na maneno na simu ikakatika.

Je, ushauri wako ni upi?