Patanisho:Jamaa alia kuachwa na mkewe baada ya mwanamume mwingine kuahidi kumfungulia hoteli

"Huwa ananiambia nimtumie pesa ya matumizi ya mtoto. Nikishatuma ananiblock," Clinton alisema.

Muhtasari

•Clinton alisema mkewe aligura ndoa yao ya mwaka mmoja baada ya jamaa kumshawishi aende akamfungulie biashara. 

•Clinton alidai mkewe pia alikuwa na mpango wa kumrudia mpenziwe wa zamani aliyekuwa amezaa mtoto mmoja naye.

Ghost na Gidi
Ghost na Gidi
Image: RADIO JAMBO

Jamaa aliyejitambulisha kama Clinton Nyongesa ,26, kutoka Nakuru alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mke wake Vivian Sawinja ,23, ambaye alimtema mapema mwaka uliopita.

Clinton alisema mkewe aligura ndoa yao ya mwaka mmoja baada ya jamaa mwingine kumshawishi aende akamfungulie biashara. 

Pia alidai kwamba mama huyo wa mtoto wake mmoja pia alikuwa na mpango wa kumrudia mpenziwe wa zamani aliyekuwa amezaa mtoto mmoja naye.

"Nilipata anaongea na jamaa fulani kwa simu. Alikuwa jamaa ambaye alikuwa amemwambia aende amfungulie  hoteli wafanye pamoja. Vivian akaanza kujipanga hapo akaondoka akaenda kwa huyo jamaa," Clinton alisimulia.

Aliendelea, "Vivian alikuwa anatumia simu yangu. Alikuwa anatuma picha kwa huyo jamaa. Niliona meseji zao... Sku moja nilikuwa nimeenda sokoni, kurudi nikapata hayuko. Nilipata ameacha mlango na geti wazi. Baadaye niliambiwa ako kwa jirani. Baadaye tena huyo jamaa alikuja na wakaenda na yeye. Nilijariubu kuongea na yeye nimuombe msamaha akaniambia amenisamehea na akasema nimtumie nauli akuje. Nilituma nauli akuje lakini hakuja. Ilifika mahali akaniblock."

Licha ya ku'blockiwa kwenye simu, Clinton alisisitiza angependa kurudiana na mwanadada huyo akisema, "Nilikuwa nimezoea yeye na nilikuwa nampenda. Yeye huwa ananiambia hana mtu lakini najua lienda kwa huyo jamaa."

Pia alizungumza kuhusu jinsi alivyofanya juhudi nyingi za kumshawishi mkewe arudi ila zote zimeangulia patupu.

"Huwa ananiambia nimtumie pesa ya matumizi ya mtoto. Nikishatuma ananiblock," alisema.

Juhudi za kumpatanisha Clinton na Vivian hata hivyo hazikufua dafu kwani mama huyo wa watoto wawili hakupatikana kwenye simu.

Alipopewa fursa ya kumuongelesha mkewe hewani, Clinton alisema, "Tafadhali Vivian nakuomba ukuje tuishi na wewe. Nakupenda kama mke wangu."