Patanisho: Jamaa ashuku amepatikana aki'cheat baada ya mkewe kutoroka kimya kimya

Laureen alipopigiwa simu aliweka wazi kwamba hana nia ya kurudiana na Samuel.

Muhtasari

•Samuel alisema uhusiano wake wa mwaka mmoja ulisambaratika wakati mkewe alipoenda nyumbani na kukataa kurudi.

•Laureen alieleza kwamba anahitaji muda wa kutulia nyumbani huku akimshtumu mpenzi huyo wake kwa kuwa na mipango wa kando.

GHOST NA GIDI STUDIONI
GHOST NA GIDI STUDIONI GHOST NA GIDI STUDIONI
Image: RADIO JAMBO

Samuel Ochieng' ,23, kutoka Kisumu alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mke wake Laureen Akinyi ,22, ambaye alikosana naye mwezi uliopita.

Samuel alisema uhusiano wake wa mwaka mmoja ulisambaratika wakati mkewe alipoenda nyumbani na kukataa kurudi.

Alisema mkewe alienda nyumbani kwa ajili ya Krismasi na amekataa katakata kurudi kwao licha ya juhudi zote alizopiga.

"Laureen alikuwa anataka kuenda nyumbani Krismasi. Lakini sikuwa tayari. Nilitaka aende tarehe moja. Alienda na hajarudi. Nikimuuliza anasema anarudi, hadi nilimtumia nauli.Hajawahi kurudi. Sijui kama nilimkosea," Samuel alisema.

Baada ya kusukumwa na Gidi akiri ukweli wote, Samuel alikiri kwamba ni alikuwa na mpango wa kando.

"Ni kweli nilikuwa naongea na mwanadada mwingine. Lakini nilikuwa nawajibika nyumbani. Nimeachana na huyo mwanadada Alienda bila kuleta shida yoyote. Nilishuku tu anataka aende nyumbani juu ya huyo msichana. Nilishuku nimepatikana," Samuel alisema.

Aliongeza, "Anasema anarudi lakini bado. Anasema tutaenda kwao 2025 ama 2027. Anasema tusipate mtoto sasa, tupate 2027."

Laureen alipopigiwa simu aliweka wazi kwamba hana nia ya kurudiana na Samuel.

Alieleza kwamba anahitaji muda wa kutulia nyumbani huku akimshtumu mpenzi huyo wake kwa kuwa na mipango wa kando.

"Yeye ndiye ananisumbua. Yeye akitoka harudi mapema. Anapenda wasichana. Nilitoka kama naenda nyumbani. Bado napumzika, sitaki mambo ya wavulana," Laureen alisema.

Samuel alijaribu kumuomba mkewe, "Nilikuwa naomba anisamehe arudi nyumbani tuendelee kuishi. Unataka nikuache utulie kwa muda gani."

Laureen alisema, "Siwezi rudi. Mimi bado niko nyumbani. Siwezi tu kurudi.Nitaamua mwenyewe kama nitarudi. Wewe teseka tu. Ndio umeanza, bado."

Samuel alisema, "Mahali nimefika, nimefika mwisho. Huyo msichana likuwa ex wangu. Alikuwa anataka kuleta mguu akapata nyumba imejaa."

Walipopewa fursa ya kuambiana maneno ya mwisho, Laureen alisema, "Sitaki hiyo mambo ya maneno ya mwisho. Unanipigia kelele."