logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Patanisho: Mume wangu aliniacha baada ya kunipigia simu na kupata 'line busy'

Hata hivyo, bado hawakuwa wameanza kuishi pamoja.

image
na Davis Ojiambo

Vipindi01 March 2024 - 06:05

Muhtasari


  • • ". Alinipigia simu akapata niko kwenye simu nyingine na hiyo ndio ilileta shida yote. Hatukuwa tumeoana lakini tulikuwa katika mpango wa kuanza kuishi pamoja" alisema.

Katika kitango cha Patanisho asubuhi kwenye Radio Jambo, mwanadada kwa jina Ruth mwenye umri wa miaka 24 kutoka Kitale alitaka kupatanishwa na mumewe Peter.

Ruth alisema wamekaa kwa ndoa kwa miaka 2 na wana mtoto mmoja na tatizo hilo lilianza Desemba mwaka jana.

Ruth alisema mumewe alimpigia simu akampata ako kwenye simu nyingine na tatizo likaanza hapo ambapo alimkasirikia.

Hata hivyo, bado hawakuwa wameanza kuishi pamoja.

“Alikuwa ananishuku sana, akiona hata nikizungumza na mtu. Alinipata na mtu tukizungumza tu kijamii. Alinipigia simu akapata niko kwenye simu nyingine na hiyo ndio ilileta shida yote. Hatukuwa tumeoana lakini tulikuwa katika mpango wa kuanza kuishi pamoja. Ninataka tu anisamehe kama hiyo simu ilimkwanza, kwani bado mimi nampenda,” Ruth alijieleza.

Peter alipopigiwa simu, alipatikana kwenye kelele sana na hivyo kuifanya vigumu kuwasiliana naye.

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved