Patanisho: "Akikupatia pesa uende soko anataka change, ata kama ni 5 bob" Mwanadada amlalamikia mumewe

"Ukivaa nguo anasema umevaa nguo fupi. Nilichoka tu. Alafu hataki uongee na watu," Caroline alilalamika.

Muhtasari

•Patrick alisema ndoa yake ya mwaka mmoja ilivunjika Desemba kufuatia mizozo ya kinyumbani na fitina za majirani.

•Carolyne alipopigiwa simu alibainisha kuwa mumewe ni mtu mwenye wasiwasi wa mahusiano na mwenye masharti tele.

Ghost na Gidi
Ghost na Gidi
Image: RADIO JAMBO

Jamaa aliyejitambulisha kama Patrick Nandwa ,29, kutoka Kakamega alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na aliyekuwa mke wake Carolyne Tuti Ayuma ,22, ambaye alikosana naye takriban miezi mitatu iliyopita.

Patrick alisema ndoa yake ya mwaka mmoja ilivunjika Desemba kufuatia mizozo ya kinyumbani na fitina za majirani.

Pia alieleza kwamba kuna wakati aliwahi kushikwa na polisi akamuomba mkewe amtembelee ila akakosa, jambo ambalo halikumpendeza.

"Mimi nafanya kazi Limuru. Tulipatana na Carol kazini. Kuna wakati nilishikwa nikiwa kazi ya ulinzi. Niliposhikwa nilikuwa nataka akuje anitembelee, akuje nimwambie vile kuko. Nilikuwa nimewekwa rumande Nikimpigia simu hakuwa anashika. Nilipotoka nikamwambia tunafaa tupatane tuongee, hatukuelewana," Patrick alisema.

Aliongeza, "Tumekuwa na misukasuko na majirani, mara anaenda kwa binamu yangu anaambiwa maneno. Pia fitina za majirani. Hajaniambia shida ni nini."

Carolyne alipopigiwa simu alibainisha kuwa mumewe ni mtu mwenye wasiwasi wa mahusiano na mwenye masharti tele.

"Huyo ni jamaa tu ako na mambo yake. Ako insecure. Alafu anataka vitu haziko zikuwe. Na maneno tu hivi. Ukivaa nguo anasema umevaa nguo fupi. Nilichoka tu. Alafu hataki uongee na watu," Carolyne alisema.

Aliongeza, "Nilimwambia anipee muda, sijui mbona ako na video. Aliniambia atanipeleka Radio Jambo nikamwambia aache ujinga."

Patrick alimwambia, "Nataka tujenge ndoa yetu, watu wengine wasiingilie. Nilikupeleka kwa Radio Jambo juu nakupenda."

Carolyne alisema, "Nilikwambia unipee muda nifikirie...  Unanipeleka speed sana. Nilikwambia kama una haraka wee oa tu, sina shida.. Ako na mbio, ati mara anataka mtoto. Kuongea na watu ni shida. Alafu kuprovide."

Pia alilalamika kuhusu mumewe kutowajibikia mahitaji ya nyumbani na kudai salio kila mara akimtuma sokoni.

"Akikupatia pesa uende soko anataka change, ata kama ni 5 bob. Alafu hataki mtu afanye kazi. Anataka akikuja akupate tu kwa nyumba. Nyumba yenyewe haina TV," alisema.

Alimbainishia Patrick kuwa hampendi tena akisema, "Mimi roho yangu ilitoka kwake. Sitaki ndoa mimi. Vitu zenye alinifanyia zilifanya nikamchukia kabisa."

Patrick pia alimlalamikia mwanadada huyo akisema, "Shida nilikuwa nayo ni vile nilipata namba ya jamaa kwa simu yako, na pia vile bibi ya cousin yangu akikuitia wanaume kwa supermarket. Mimi sina shida ingine."

Aliongeza, "Alipata ujauzito wakati tukiwa kwa hayo mahusiano na hakuniambia. Akapata tena ujauzito na hakuniambia. Lakini nikavumilia."

Patrick hata hivyo alimhakikishia mpenzi huyo wake kuhusu mapenzi yake kwake licha ya kuachana.

"Caroline mimi nilikupenda na roho moja. Wewe kama utakaa chini uone turudiane ni sawa. Mimi sioni vile nitaanza kurukaruka. Naomba unisamehe, mtu hukosea," alisema.

Je, una maoni yepu kuhusu Patanisho ya leo?