logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Patanisho: Jamaa aachwa baada ya kupost rafikiye wa Qatar mnamo siku ya Valentine's

Maureen hata hivyo, alimtaka apige hatua ya kufika nyumbani kwao ili washiriki mazungumzo pamoja na wazazi.

image
na Radio Jambo

Yanayojiri21 May 2024 - 05:32

Muhtasari


•Kelvin alisema ndoa yake ya miaka miwili ilivurugika Februari 2022 wakati mkewe alipotoroka baada ya kuona mazungumzo yake ya simu na mwanadada mwingine.

•Kelvin alisitiza kwamba tayari amekatiza mawasiliano na mwanamke ambaye alikuwa akichat naye na kusema angetaka kujua msimamo wa Maureen.

GHOST NA GIDI STUDIONI

Kelvin Mwenda ,27, kutoka Meru alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mke wake Maureen Gatwiri ,23, ambaye alikosana naye zaidi ya miaka miwili iliyopita.

Kelvin alisema ndoa yake ya miaka miwili ilivurugika Februari 2022 wakati mkewe alipotoroka baada ya kuona mazungumzo yake ya simu na mwanadada mwingine.

Alisema mkewe alikasirika baada ya kuona amepost mwanamke mwingine mnamo siku ya Valentine's, jambo lililofanya agure ndoa.

"Ilikuwa siku ya Valentine vile mtu hupost marafiki, akaona nimepost mtu ambaye nimeishi kuongea na yeye. Alikuwa ameona text zangu na yeye. Huyo mwanamke alikuwa Qatar wakati huo.Tulikuwa tunachat tu text za kawaida. Mke wangu alikasirika tukagombana usiku alafu siku ifuatayo akaenda kwao," Kelvin alisimulia.

Aliendelea kuelezea, "Kabla hata tupatane na bibi yangu, tulikuwa marafiki na huyo mwanamke. Hatukuwa katika mahusiano. Ni ile tumetoka mbali tunaweza kuzungumza chochote. Hakutaka kuelewa. Alikuwa anajua, lakini mke wangu ni mtu mwenye wivu. Nilikuwa nimeacha lakini ile kuchat haingeisha. Hapo ndio shida yote ilitoka. Nikatafuta wazazi. Mama yangu akajaribu kuongea na yeye, lakini akasema amechoka na ndoa anataka kuenda. Aliniacha mtoto akiwa mdogo, sasa ako na miaka mitatu."

Kelvin alisitiza kwamba tayari amekatiza mawasiliano na mwanamke ambaye alikuwa akichat naye na kusema angetaka kujua msimamo wa Maureen.

"Nilituma kujua msimamo wake. Hakuna haja ya mtu kukaa na matumaini na mwenzake hana mpango. Tumekuwa tukiongea na nikifuatilia naskia tu yuko nyumbani. Sikuwa na haraka ya kutafuta mwingine kwa sababu upendo sio kitu ya kuchezea," alisema.

Maureen alipopigiwa simu aliweka wazi kwamba hana shida kurudiana na mzazi mwenzake.

Hata hivyo, alimtaka apige hatua ya kufika nyumbani kwao ili washiriki mazungumzo pamoja na wazazi.

"Mimi sina shida lakini kwanza ningependa akuje nyumbani kwa sababu sasa niko nyumbani na siwezi kutoka hivihivi. Ndio angalau tuongee na wazazi tuelewane pande zote. Mimi sina shida," Maureen alisema.

Kelvin ambaye alisikika kujawa bashasha baada ya hakikisho la mkewe alisema, "Nimefurahi. Nashukuru sana. Nimejua msimamo wake na hiyo tu ndo nilitaka. Kuenda nyumbani kwao sio shida kwa sababu nimeenda mara nyingi. Nampenda sana na ningependa turudiane tukae maisha yetu pamoja."

Je, ushauri ama maoni yako kuhusu Patanisho ya leo ni yepi?


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved