Jamaa aachwa kwa sababu ya uongo na kukosa maendeleo

Melody Chepkemoi,26 amemtaja Daniel Langat kutoka Kericho kama jamaa muongoo baada ya kuishi naye kwa takriban mwezi mmoja huku akidai kuwa hatarudi tena kwake.

Muhtasari

•Daniel Langat alikosana na bibi yake Melody Chepkemoi Novemba 2023 baada ya kumshuku kuwa na mwanaume mwingine.

•Melody alisema kuwa hio ilikuwa uongo na ameamua kuachana na Daniel kutokana na tabia zake za uongo baada ya kumsoma kwa takriban mwezi moja walipokuwa pamoja.

Gidi na Ghost studioni
Image: RADIO JAMBO

Jamaa aliyejitambulisha kama Daniel  Langat,35 kutoka Kapsoit,Kericho alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mke wake Melody Chepkemoi mwenye umri wa miaka 26.

Daniel alisema kuwa alikuwa ameoa hivi majuzi lakini akakosana na bibi yake Novemba 2023.Alisema kuwa akitoka kwenda kazini,bibi yake huenda kwa jamaa mwingine ambaye ni jirani yake.

"Huyu Melody tulioana na yeye mwaka jana ,na wakati wa kufukuzana na hali ya maisha,kumbe alikuwa na boyfriend hapo karibu.Baadaye majirani wakaanza kuniambia mbona mke wako anaenda hivi na hivi.Ndani ya wiki moja alikuwa  kwa huyo boyfriend wake.Niliacha tu afanye mambo yake  yote na baada ya hapo ,akarudi nyumbani nikamwambia arudi kwao bila kumfanyia chochote."

Hata hivyo walijaribu kuongea na kusikizana kabla ya kutofautiana tena baada ya muda muchache.Vile vile Daniel alijaribu kuongea na mamake Melody huku akimtaka waongee na Melody ili kuelewana.

"Tuliongea  na watu wa familia yake ndugu zake,dada zake lakini inaonekana yeye ndiye mkorofi kidogo..." Daniel alisema.

 

Melody  alipopigiwa simu alisema kuwa  yeye hawezi kurudi kwa kuwa Daniel alikuwa ameoa bibi mwingine.

"Mimi venye niltoka hapo sikufuatilia maisha yake. Yeye mwenyewe alikuwa ananitumia ujumbe kwa simu akisema kuwa amepata bibi mwingine,hanitaki tena.Mimi niliona hio kama utoto kwa sababu  sikuwa nashughulika nazo, saa zingine alikuwa ananitusi kupitia jumbe za simu.Katika hali yangu ya kuwa mtu mkubwa ,sikutaka kujibizana naye.Niliamua kumfungia simu na kumblock."

Hata hivyo Daniel alisisitiza kusamehewa. "Hizo zilikuwa hasira za nyuma ,ndo maana sasa naomba msamaha ili turudiane hio ni mambo yaliyopita yafaa tugande yajayo." Daniel alisisitiza.

Melody aliongeza kuwa yeye hakuwa na boyfriend. "Wakati tulikuwa tushaoana na Daniel sikuwa na boyfriend,nilkuwa naenda tu kukaa kwa jirani mwanamke huku yeye akifikiria nilikuwa na boyfriend."

"Nimemsoma kwa muda kidogo tulikuwa na yeye takriban mwezi moja ,yeye si mtu wa maendeleo nishaamua ,sirudi huko tena..."

Aidha Daniel aliendelea kujitetea huku akitaka Melody amwambie ni kwa nini anamwona kama mtoto na mtu ambaye hana maendeleo.

"Mimi ni mwanariadha na saa zingine nikitoka  mazoezini majukumu ni mengi,Melody yafaa arudi labda tu aelezee ni nini aliona kitu mbaya kwangu..." Daniel alisema.

"Huyo mtu tukikutana ,alikuwa na watoto watatu.Alikuwa anaambia watoto wasiniambie chochote kumhusu.Nilianza kuzoeana na watoto na wakaanza kufunguka siri zote.Kuna siku aliniambia ameenda kwa wajomba wake ,mimi nilkuwa nyumbani kwetu nikaamua niende kwake bila kumwambia...on the way nikija nilikutana na msichana wake akaniambia kuwa baba yake hakusafiri na alikuwa tu nyumbani.......tangu hio siku nilijua kuwa huyu jamaa ni muongo tu totally..." Melody alisema.