Patanisho:Mama amsamehe bintiye kwa tabia ya ulevi na usherati

Irene Nelly alikisiwa na mamake kuwa na tabia chafu ikiwemo ulevi pamoja na kumdharau babake mlezi jambo ambalo lilifanya wawili hao kukosana toka mwaka wa 2020.

Muhtasari

•Irene alisema kuwa alikosana na mamake baada ya babake kurudi kutoka gerezani na kumkumbatia jambo ambalo halikumfurahisha mama yake kulingana na Irene.

•Mamake Irene alipopigiwa simu alisema kuwa Irene alikuwa anamdharau babake mlezi jambo ambalo lilifanya mama kukasirika na pia tabia zake chafu za ulevi na usherati.

Gidi na Ghost studioni
Image: RADIO JAMBO

Irene Nelly ,30 kutoka Kaburengo,Bungoma alituma ujumbe akitaka kupatanishwa na mama yake Jane Kasevali mwenye umri wa miaka 50 baada ya kukosana mwaka wa 2020.

Irene alisema kuwa walikosana na mama yake  baada ya babake kushikwa juu ya ajali na mama yake alimuamuru kuondoka nyumbani baada ya baba yake kuachiliwa kutoka gerezani kwa kumkumbatia alipofika nyumbani.

"Baba yangu alifungwa kwa kifungu ya miaka sita.So,ikawa baba anarudi nyumbani.Mama akaniambia nitafute nyumba yangu kwa kuwa babangu anarudi nyumbani.Nilimuuliza kwa nini akasema tu hakuna.Ikawa hivo baba akarudi,hizi movies tunapenda kuwatch za Nigeria,venye nilihug babangu,ni kama mamangu alikasirika.Kuanzia hapo chuki ikaanza kati yangu na mamangu.Mama akaanza kusema eti nimeungana na brother yangu tukaiba vitu nyumbani,mambo mingi tu.Hatuongeleshani ,inabidi nimedanganya bwanangu eti nmeenda nyumbani lakini huwa naenda kukodisha nyumba kwa mwezi moja ,then narudi kwangu..."

Irene aidha alisema kuwa alikuwa na miaka 28 baada ya babake kurudi kutoka gerezani.Alikuwa amekosana na bwana yake na kurudi nyumbani kukaa na mamake.

"Mama yangu si mtu wa kusikiza ,anaomgea mambo mengi.Mum aliniambia hadharani mbele ya dad kuwa haoni kama ananitaka.Huyo babangu si babangu mzazi,ni baba wa kunilea.Mum akiniona ananiona kama shetani..."

Irene aliongeza kuwa ndoa yake inayumba na angependa kupatanishwa na mama yake ili arudi kwa maisha yake ya kawaida.

"Bwana akisema anataka kwenda kwetu ataingia wapi ,ningependa tu kujua kikubwa nilifanya na niko tayari kumwomba mamangu msamaha...'

Mamake Irene alipopigiwa simu alisema kuwa Irene alikuwa na makosa kubwa sana kwa babake,lazima aombe babake msamaha kwa kuongea vibaya.

"Maneno aliyoongea kwa babake yalikuwa machafu sana.Huyo baba mwenye anadharau amenisaidia sana kwa maisha ,ameninunulia shamba na kila kitu.Nikiwa na huyo bwana huyu Irene alikuwa na miaka saba,kwa sasa ameolewa ako na watoto na anadharau huyu bwanangu.Makosa alifanyia baba yake ni kubwa.lazima aombe baba yake msamaha .Alaf mambo ya ulevi , analewa anarudi nyumbani akinitusi.Ananikosea heshima sana,awache pombe na akuje aombe babake msamaha.Lazima pia ajifunze kukaa na familia yake.."

Mamake Irene aliongeza;

"Anafanya usherati karibu na hapa kwa jirani...na ameleta watoto wake kwangu."

Aidha,Irene aliendelea kusisitiza kuwa babake alimsamehe ,'Mimi mambo ya pombe niliacha kitambo ,hata huku kakamega penye naishi huwa sionji kidogo.Kitambo nilikuwa naonja nikiwa na stress na hio mama anajua."

Mamake Irene alikiri kumsamehe huku akitaka azuru familia yote aiombe msamaha. "Ajipange akijua yeye ni mwanamke,lazima akuje aombe msamaha dada zangu wote msamaha ,awache umalaya ,aombe msamaha na akuje tukae kikao.Kama ni kukaa na bwanake afanye hivo na awache umalaya."