Patanisho: Binti arukwa na mpenziwe aliyedai kutomjua

Beryl alidai kuwa alimkosea George baada ya kumrushia cheche za matusi ila George alipopigiwa simu alisema kuwa yeye hamfahamu Beryl.

Muhtasari

•Beryl alitaka kusamehewa na George baada ya kumrushia matusi kwa simu huku akidai kuwa George alikuwa akimsaidia kimaisha.

•Wawili hao walikosana majuma mawili yaliyopita ila George alipopigiwa simu alikanusha kuwa yeye hamfahamu Beryl.

Gidi na Ghost studioni
Image: RADIO JAMBO

Binti mmoja anayejulikana kama Beryl ,22 alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mpenzi wake George, 27 anayeishi Mombasa baada ya kukosana majuma mawili yaliyopita.

Beryl alisema kuwa alikosana na mpenzi wake George baada ya kumtukana na kwa sasa hawaongeleshani akidai kuwa alikuwa akimsaidia kimaisha.

"George alikuwa mpenzi wangu lakini tukaja tukakosana.Kuna msichana mmoja tulikuwa tunaongea na yeye facebook,kumbe alikuwa ex wa George.Mimi nilipouliza George kuhusu huyo msichana alinikasirikia na kuniuliza ni kwa nini nilikuwa naongea na huyo msichana.Kutoka hapo nikakasirika pia na nikaanza kumtusi...."

Aliongeza, "Baada ya kukasirikiana ,aliniambia nimpee wiki moja afikirie kama atanisamehe,lakini tangu hapo hajakuwa akiniambia chochote.Juzi nilimpigia simu kwa namba nyingine nikijaribu kumuomba msamaha lakini alinyamaza bado na hakuniambia chochote ..."

Beryl alithibitisha kuwa mpenzi wake George alikuwa akiongea na mpenzi wake wa zamani  baada ya kufuatilia 'comments' kwenye ukurasa wake wa Facebook.

"Niliingia kwa account yake nikafuatilia comments ...kuuliza yule dem wake akacheka tu.Tulikuja tukawa marafiki na huyo 'ex' wa George baadaye..."

George alipopigiwa simu na kudai kuwa angependa kuombwa msamaha alisema; "Niko  busy kwa gari...niko kwa highway"

Hata hivyo mtangazji Gidi alimfichulia kuwa Beryl ndiye ambaye alitaka kumuomba msamaha,George  alikanusha kuwa yeye hamjui Beryl

"Simjui huyo" George alisema.

Beryl kwa upande wake alidai kuwa yeye alitaka tu kuomba msamaha na kuongeza kuwa George alikuwa anadanganya na kumwita mkora baada ya kukanusha kuwa hamfahamu.

Je,una maoni gani kwa patanisho ya leo?