Patanisho:Binti asamehewa baada ya kumpokonya rafiki yake mpenzi

Lydia alidai kuwa amemsamehe Amara baada ya kumpokonya mpenzi japo akitaka urafiki wao urudi sawa sharti amletee mpenzi mwingine.

Muhtasari

•Amara alipiga simu akiomba kupatanisha na rafiki yake Lydia baada ya wawili hao kukosana Februari 2024.

•Lydia alidai kuwa Amara alimpokonya bwana na hivo aliamua  kumsamehe japo ili urafiki wao udumu sharti amletee bwana mwingine.

Mtangazaji Gidi Ogidi
Image: RADIO JAMBO

Binti mmoja anayefahamika kama Amara,24 kutoka Nakuru alituma  ujumbe akiomba kupatanishwa na rafiki yake Lydia Nyambese kutoka Kisii baada ya kukosana Februari 2024.

Amara alisema kuwa alikosana na rafiki yake baada ya rafiki yake  kuamua kumnyamazia kighafla tangu aondoke mjini Kisii.

"Nilikuwa naishi Kisii nikaamua kuondoka kuelekea Nakuru na tangu wakati huo hatujakuwa tukiongea na rafiki wangu Lydia.Kwa sasa sijafahamu tatizo ni lipi ,ningependa tu kujua ili turudiane.Kila ninapopiga simu huwa hashiki.Kukosana na rafiki ni 'so much painful'  kuliko kushinda kukosana na mpenzi wangu..."

Amara aliongeza kwa kusema kuwa mtu yeyote wa karibu ni rafiki na wala si mpenzi hivo yeye anapendelea kukosana na mpenzi wake na wala si rafiki yake.

Lydia alipopigiwa simu alidai kuwa Amara alimpokonya mpenzi wake na hivo kusababisha urafiki wao kugoma.

"Huyo msichana nilimsaidia,akachukua bwana wangu,ningefanyeje sasa? Alikuwa anaelezea bwana yangu eti mimi ni mbaya na eti simpendi,kuwa nina wanaume wengine.Niko na jumbe za simu ambazo alikuwa anamtumia bwana yangu. Hadi anamwambia eti  yeye ni mzuri kuniliko...."

Aidha Lydia alisema kuwa hajui kama sa hii Amara yupo na bwana yake wa kitambo na kudai kuwa yafaa kusema.

"Bwana yangu aliamua kutoka na kuniacha na mtoto" Lydia alisema.

Hata hivyo Amara alidai kuwa haelewi stori zinazosemwa. "Kwa kweli mimi sielewi...mimi niko na bwanangu na hakuna jinsi nitachukua bwana ya mtu..."

Amara,aliamua kumwomba msamaha Lydia huku akisisitiza kuwa yeye hakumpokonya bwana "Mimi sikujua nakosea hivo naomba msamaha,urafiki wetu ni muhimu sana kuliko kitu chohote kile."

Lydia alikubali kumsamehe,"Mimi nishakusamehe ila uishi maisha yako na usinifuatilie tena ,ukitaka urafiki wetu udumu kama hapo awali,unitafutie bwana mwingine kama yule wa zamani kwa sababu alikuwa ananipa mataji."

Amara alijaribu kujitetea kwa kusema kuwa yeye alikuwa anaongea na bwanake  Lydia kuhusu tu mambo ya kawaida ila Lydia alishikilia msimamo wake.

Je,una maoni gani kwa patanisho ya leo?