Patanisho: "Nitakaa aje miezi 3, 4 bila kubadilisha oil?!" Jamaa alalamika mkewe kukwama nyumbani kwao

Sifuna alilalamika sana kuhusu jinsi anavyoteseka bila mkewe kuwa karibu.

Muhtasari

•Sifuna alisema kuwa ndoa yake ya miaka minne ilisambaratika mwezi wa tatu wakati alipoenda nyumbani kwao na kukosa kurudi.

•"Mimi ni mwanaume, mimi ni kijana bado sijazeeka. Mwanaume nitakaa aje miezi tatu, nne bila kubadilisha oil!" Sifuna alilamika.

GHOST NA GIDI STUDIONI
GHOST NA GIDI STUDIONI GHOST NA GIDI STUDIONI
Image: RADIO JAMBO

Wenslaus Sifuna ,35, kutoka Bungoma alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mke wake Gladys Katumbela ,33, ambaye alikosana naye mapema mwaka huu.

Sifuna alisema kuwa ndoa yake ya miaka minne ilisambaratika mwezi wa tatu wakati alipoenda nyumbani kwao na kukosa kurudi.

"Mke wangu nimekaa naye zaidi ya miaka nne. Nilimpata na watoto watatu, na mimi nilikuwa na wangu watatu. Mama yake alikufa mwaka jana, tukaanza kusumbuana. Alikuja kwangu na mtoto mmoja, wengine wawili walikuwa na baba watoto, walikuwa wameachana," Sifuna alisimulia.

Aliendelea, "Baada ya kuzika mamake, alisema mtoto anafaa kupelekwa nyumbani kutahiriwa, ilikuwa mwaka huu mwezi wa tatu. Bado hajarudi. Nilichukua huyo mtoto kama mtoto wangu. Alitoka kwa ndoa ya kwanza 2013. Mtoto wake wa mwisho alikuwa mdogo, Hadi nilimpeleka shule."

Sifuna alidai kwamba angependa kujua msimamo wa mkewe akibainisha kwamba amechoka sana kungoja.

Gladys alipopigiwa simu, Sifuna alichukua fursa hiyo kulalamika kuhusu jinsi anavyoteseka bila mkewe kuwa karibu.

"Mahali nimekaa nimevumilia nikachoka, Ningependa kujua msimamo wake. Nataka kujua ukweli wake nijue nachukua hatua gani. Tangu uniache hapa, mambo yangu mengi yamesimama na hayaendi sawa. Mimi ni mwanaume, mimi ni kijana bado sijazeeka. Mwanaume nitakaa aje miezi tatu, nne bila kubadilisha oil!" Sifuna alilamika.

Gladys alisema, "Huyo mwanaume alikuwa anasema hawezi kupeleka mwanamke kwa radio. Nitarudi ata kama sio saa hii. Anisubiri kidogo. Kuna shughuli nilienda, ata yeye anajua."

"Huyo mwanaume najua ananipenda. Mwambie asubiri. Alafu achukue muda akuje nyumbani kwa wazazi wangu. Kama kuna shida, aeleze," aliongeza.

Sifuna alisema kwamba angempigia mkewe simu baadaye ili waweze kuzungumza zaidi.

"Nilikuchukua kama mke wangu. Wa dhati na wa ndani sana. Popote unapoenda ujue nakupenda kama mke wangu. Ukitaka kurudi kwako wakati wowote ujue milango wazi.Nakupenda kuliko pesa yenye natafuta kila siku," alimwambia mkewe.

Gladys alimwambia mumewe, "Kama sikuwa nakupenda, singeshika simu ya Radio Jambo. Mengine upange uje nyumbani tuzungumze."