Patanisho: Mwanamke amuonya kakake mdogo dhidi ya kumuita dada baada ya kumuongelesha vibaya

"Wewe ndiye ulikuwa mang'aa. Uliniongelesha vibaya na mimi ndiye mkubwa wako," Jane alimwambia kakake.

Muhtasari

•Stephen alisema uhusiano wake na dadake uliathirika Aprili mwaka huu baada ya kumtupia cheche za maneno mkubwa huyo wake.

•Jane alikubali kumsamehe kakake mdogo na kuahidi kutofikisha maneno yake kwa mkewe kila wakati.

Gidi na Ghost
Image: RADIO JAMBO

Stephen Mutuku ,26, kutoka Makueni alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na dada yaje Jane Mutuku ,31, ambaye alikosana naye mapema mwaka huu.

Stephen alisema uhusiano wake na dadake uliathirika Aprili mwaka huu baada ya kumtupia cheche za maneno mkubwa huyo wake.

Alidai kwamba dadake alikuwa alikuwa akimwambia mkewe kuhusu kila kitu ambacho alikuwa akifanya.

"Nilioa 2022 nikakuja tukakaa na bibi. Tulikosana akaenda kwao. Baada ya yeye kuenda, nikifanya kitu nyumbani, dada yangu anamwambia. Nilikasirika nikamuuliza dada yangu mbona anaambiana mambo yangu," Stephen alisema.

Aliongeza, "Nilifuatilia nikajua huwa wanachat Facebook. Bibi alinitumia screenshots nikajua ni dada yangu alikuwa anamwambia. Tulikosana na dada akaniambia nisiwahi kumuita dada tena. Mke wangu alirudi. Dada yangu aliblock hadi mke wangu."

Jane alipopigiwa simu, Stephen alichukua fursa hiyo kumuomba msamaha na kumsihi warejeshe uhusiano mzuri.

"Nilitaka tusameheana tuishi vile tulikuwa tunaishi," Stephen alisema.

Jane alisema, "Wewe ndiye ulikuwa mang'aa. Uliniongelesha vibaya na mimi ndiye mkubwa wako."

Hata hivyo, alikubali kumsamehe kakake mdogo na kuahidi kutofikisha maneno yake kwa mkewe kila wakati.

"Nimemsamehe. Atanipigia mimi sijamblock,, Kama hiyo ndio shida, itaisha," Alisema Jane.

Stephen alisema, "Jane mimi nakupenda kama dada yangu. Ningependa turekebishe mahusiano yetu kama ndugu."

Jane alimalizia kwa kusema, "Pia mimi  nimekusamehe kama kaka yangu."