•Bi Catherine alisema alikuwa kwa ndoa na Bw Masakwi kwa miaka minne, wakajaliwa watoto wawili kabla ya kutofautiana na kutengana.
•Masakwi hata hivyo alitupilia mbali madai ya mzazi huyo mwenzake akibainisha kwamba tayari ana mume mwingine.
Bi Catherine Lisamba ,56, kutoka Vihiga alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na baba watoto wake Joseph Masakwi ,61, ambaye alikosana naye miaka 30 iliyopita.
Bi Catherine alisema alikuwa kwa ndoa na Bw Masakwi kwa miaka minne, wakajaliwa watoto wawili kabla ya kutofautiana na kutengana.
"Sitaki kurudiana. Tuliachana naye watoto wakiwa wadogo kwa sababu ya mambo yake ya hapa na pale, alikuwa analeta wanawake. Watoto wanajuana naye. Hata wanajuana na mama ya kambo. Nimeona hakuna haja ya kumwekea uchungu kwa roho, tusameheane," Bi Catherine alisema.
Alidai kwamba hajawahi kuolewa tena baada ya kutengana na Bw Masakwi miongo mitatu iliyopita.
"Mimi ndio nilitoka nikaenda zangu kwa sababu niliona ningekufa na stress. Bado niko pekee yangu, sikutaka kuoeleka. Yeye aliendelea kuoa saa hii ako na bibi watatu. Watoto wake ata hawahesabiki," alisema.
Bw Masakwi alipopigiwa simu, Catherine alichukua fursa hiyo kumuomba msamaha na kumsihi wawe na uhusiano mzuri.
"Sio eti kwa sababu nataka turudiane, ni kwa ile grudge nimekuwa nayo miaka 30 imepita. Nimeona nikuweke kwa radio jambo, kama kuna mahali nilikukosea, nakuomba msamaha. Na wewe mahali ulinikosea, wewe unajua ili wajukuu waelewe kwa nini tunakaa tofauti. Nakuomba unisamehe mahali nilikukosea, na mimi mahali ulinikosea uniombe msamaha nikusamehe," Catherine alisema.
Bw Masakwi ambaye alisikika kushangazwa sana na hatua ya mzazi huyo mwenzake alisema, "Mimi najua ni mama ya watoto, sina shida na yeye. Mimi sijui kama nimemkosea. Najua yeye ni mama ya watoto tuko katika mahusiano mema. Lakini kwa upande wangu sina chochote ndani ya roho."
Bi Catherine aliendelea kulalamika akisema, "Hata wazazi wangu walipokufa, hakuja mazishi. Hata hakuwahi karibia kaburi zao ilhali hao wazazi walikuwa wanamkaribisha nyumbani na kumpikia."
Alimwambia Bw Masakwi, "Nilikutambua kama mume wangu. Wewe ndiye ulikuwa bwana wangu wa kwanza. Wakati tuliacahana nilikasirika sana ata sikuwahi kuoleka tena kwa sababu ya uchung. Nakupenda kama baba watoto."
Masakwi hata hivyo alitupilia mbali madai ya mzazi huyo mwenzake akibainisha kwamba tayari ana mume mwingine.
"Huyo mama ameoleka. Anasema uongo. Mtu wa kusema uongo sipendi. Tulikuwa marafiki, tukazaa watoto. Yeye ameoleka, ana mume Mkikuyu wanakaa naye. Alitoka Afrika Kusini, nikaenda kwao, mama yake akanifukuza akasema nimefuata pesa ya mtoto wake.Wewe nakupenda aje na uko na bwana. Bwana yako akisikia nikisema hivyo alafu? " alisema Masakwi.
Bi Catherine alisema, "Mimi nilitaka uhusiano wangu naye uwe sawa. Sweetheart, Ukiwa na kitu yoyote unaweza kunisaidia kama mama watoto unisaidie. Nakupenda kama baba watoto."
Bw Masakwi hata hivyo alisema, "Mambo ya kurudiana, saa hii mimi niko na wanawake sita. Hatujawahi kukaa naye. Alikuwa rafiki tukazaa mtoto."
Je, ushauri ama maoni yako kuhusu Patanisho ya leo ni yepi?