• "Pauline jana tuliongea na yeye asubuhi ikafika saa nane nikapata ameniblock.. aliniambia alipigiwa simu eti tangu atoke kwangu wanawake 3 wameonekana kwangu"
Katika kipindi cha Gidi na Ghost asubuhi kwenye kitengo cha Patanisho, kijanaFred Clarent mwenye umri wa miaka 24, mwanafunzi wa chuo kikuu cha Maseno, Kisumu alitaka kupatanishwa na mpenzi wake Pauline Akoth mwenye umri wa miaka 22.
Clarent ambaye ako katika mwaka wa 4 chuoni alimpenda mrembo huyo mwaka uliopita wakati Pauline alikuwa mgeni chuoni katika mwaka wake wa kwanza,
Clarent alieleza kwamba walikuwa na maelewano kwamba wangeanza kuishi pamoja muhula huu lakini jana, Alhamisi, Pauline akamblock ghafla kwenye simu yake.
Alisema kwamba Pauline alimdokezea kwamba aliambiwa tangu alipoenda nyumbani mwishoni wa muhula uliopita, wanawake 3 walionekana katika nyumba ya Clarent.
“Tulipatana na yeye akiwa mwaka 1 na mimi nikiwa mwaka 3, sasa hivi niko mwaka 4. Tulikuwa tunapanga baada ya chuo tuanze maisha pamoja, tulipanga tuanze kuishi nyumba moja muhula huu. Pauline jana tuliongea na yeye asubuhi ikafika saa nane nikapata ameniblock.. aliniambia alipigiwa simu eti tangu atoke kwangu wanawake 3 wameonekana kwangu, alitoka akaenda kufanya shughuli nyingine nyumbani… sasa hivi ako nyumbani na mimi niko shule na vitu vyake viko kwa nyumba, nilitaka apigiwe simu ili turejeshe mahusiano,” Clarent alisema.
Mrembo huyo alipopigiwa simu na watangazaji Gidi na Ghost, alisema;
“Jana saa tano asubuhi alinitumia text akiniambia ako na shughuli na rafiki yake wa kike mwenye anatoka nyumbanio, na mimi nikaona hiyo text na sikumjibu nikaachana nayo nikashughulikia vitu vyangu, kufika saa nane nikapokea simu kutoka kwa jirani penye tunaishi akaniambia mpenzi wangu ameonekana na mrembo na huyu ni wa 3 tangu nitoke…nikaudhika nikambock.”
Clarent kwa upande wake alisisitiza kwamba hakumcheat mpenzi wake bali warembo alioonekana nao ni mafresha aliokuwa akisaidia kufahamu mazingira ya shule, akisema wale alioambiwa walionekana kwake hata yeye hawajui.
Hata hivyo, Pauline alisema kwa shingo upande kwamba ameridhika na maelezo yake na kuomba kupewa muda na Clarent ili kufikiria zaidi.