Patanisho live: Kevoh azima simu baada ya kuskia anatafutwa na mtangazaji Gidi (+video)

"Sina uhakika kama ako na mwanamke mwingine, namshuku tu. Sijamtembelea kwa sababu hashiki simu zangu. Naogopa," Mercy alisema.

Muhtasari

•Mercy alisema uhusiano wake wa mwaka mmoja ulisambaratika wiki mbili zilizopita baada ya kumshuku mpenziwe.

•Kelvin alipopigiwa simu, alibainisha kwamba yeye ni Kevoh kisha akakata simu baada ya kuskia anatafutwa na Radio Jambo.

Katika kitengo cha Patanisho, Mercy Wambua mwenye umri wa miaka 22 alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mpenzi wake Kevin Mwendwa ,26, ambaye alikosana naye hivi majuzi.

Mercy alisema uhusiano wake wa mwaka mmoja ulisambaratika wiki mbili zilizopita baada ya kumshuku mpenziwe.

"Ni mambo ya kumshuku tu kwa mwaka mmoja umepita. Baadaye tulikuja tukakosana. Ata simu zangu hashiki. Kutoka wiki jana hajashiki simu yangu, jana pia nilijaribu kumpigia hakushika," Mercy alisema.

Mwanadada huyo alisisitiza kwamba hafahamu jinsi alivyomkosea mpenziwe.

"Tumechumbiana kwa mwaka mmoja. Labda yeye aseme kama nilimkosea. Sina uhakika kama ako na mwanamke mwingine, namshuku tu. Sijamtembelea kwa sababu hashiki simu zangu. Naogopa. Nataka nimwambie anisamehe kama nilimkosea, turudiane," alisema.

Kelvin alipopigiwa simu, alibainisha kwamba yeye ni Kevoh kisha akakata simu baada ya kuskia anatafutwa na Radio Jambo.

Mercy alisema, "Hakuna kitu ingine naweza kumwambia. Itabidi nikubali, labda hataki mambo yangu."

Je, ushauri ama maoni yako kuhusu Patanisho ya leo ni yepi?