"Sina raha!" Mwanajeshi akubwa na stress baada ya mpenziwe kukataa kuzungumza naye

"Wajua huyo ni dadako lazima akuelewe," Yossi alimwambia Gidi.

Muhtasari

•Yossi alisema uhusiano wake wa miaka miwili uliharibika mwezi mmoja uliopita baada ya yeye kuvuruga mipango ya kukutana.

•Eve alipopigiwa simu, Yossi alichukua fursa hiyo kuomba msamaha na kumueleza mpenziwe jinsi anavyomkosa.

Gidi na Ghost
Image: RADIO JAMBO

Katika kitengo cha Patanisho, mwanajeshi Yossi Yarabi mwenye umri wa miaka 37 kutoka Mombasa alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mpenzi wake Eve ,28, ambaye alikosana naye hivi majuzi.

Yossi alisema uhusiano wake wa miaka miwili uliharibika mwezi mmoja uliopita baada ya yeye kuvuruga mipango ya kukutana.

"Wakati nilikuwa Somalia tulikuwa tunawasiliana. Yeye alikuwa kazi Kiambu. Nilipofika Nairobi nilimwambia nimefika akuje tupatane. Akasema ni ngumu niweze kuenda nyumbani kwanza. Tulikuwa tupatane. Nilikuwa nipitie kwake, simu ikazima. Nikakosa kupitia kwao nikaenda kazini kwa sababu nilikuwa nimeitwa," Yossi alisimulia.

Aliendelea, "Keshoye kumtafuta mtoto wa wenyewe amenuna hataki maneno yangu. Nikajaribu kuongea na dadangu aongee naye akawa hataki maneno yangu kabisa. Nikimtumia meseji akawa hajibu. Amenuna tu. Ananinyima raha.

Vile amenyamaza hivyo mambo si mazuri. Jana nimemtumia ujumbe akasema poa, lakini ana hasira. Watoto wa Kijaluo wanafahamu mapenzi sio kubahatisha, lakini hasira ni ya Wameru."

Eve alipopigiwa simu, Yossi alichukua fursa hiyo kuomba msamaha na kumueleza mpenziwe jinsi anavyomkosa.

"Mimi nakupenda lakini wewe unadhani nakuzingua. Vile umenizimia taa sina raha. Najua nilichofanya na najaribu kuomba msamaha hutaki kunisikia. Hamna mwanamke napenda kama wewe hii dunia," Yossi alimwambia mpenziwe.

Eve alijibu, "Ungekuwa unanipenda hungefanya ulichofanya. Ungenipigia simu uniambia kuna jambo limetokea ningeelewa. Hunitafuti, baada ya wiki mbili ndo unanitafuta, wewe unadhani mimi nitakuwa sawa. Hakuna mwanaume anakuwanga bize sana kwa mpenzi wake." 

Gidi alimtetea Yossi kwa mpenziwe hadi akakubali msahama.

"Wajua huyo ni dadako lazima akuelewe," Yossi alimwambia Gidi.

"Mimi nakupenda na hakuna mwanamke mwingine napenda humu duniani kuliko wewe. Iwe mvua iwe jua ni wewe tu," alimwambia mpenziwe.

Eve alimwambia mpenziwe, "Yossi nakupenda ata kama niko na hasira na wewe. Unipigie simu saa hizi tumalizane. Nataka attention."

Je, ushauri ama maoni yako kuhusu Patanisho ya leo ni yepi?