Patanisho: Mwanadada amshtumu kakake kwa kutaka kushiriki tendo la ndoa naye, amtangaza kwa familia

Mercy alisema aliogopa kutii wito wa kakake kwa kuwa walikuwa wao wawili tu kwa nyumba.

Muhtasari

•Mercy alisema uhusiano wao uliharibika mwezi wa sita wakati kakake alimuita kwenye chumba cha kulala, ambapo alihofia kwenda.

•"Kakangu aliniita tu kwa bedroom. Bibi yake hakuwa, mimi nikaondoka. Nikatoka nje nikapigia bibi yake," Mercy alisimulia.

Gidi na Ghost Studioni
Image: RADIO JAMBO

Mercy Wafula ,22, kutoka Eldoret alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na kaka yake Lazurus Wafula ,26, ambaye alikosana naye mapema mwaka huu.

Mercy alisema uhusiano wao uliharibika mwezi wa sita wakati kakake alimuita kwenye chumba cha kulala, ambapo alihofia kwenda.

"Kakangu aliniita tu kwa bedroom. Bibi yake hakuwa, mimi nikaondoka. Nikatoka nje nikapigia bibi yake. Mkewe alirekodi alafu akamuonyesha. Nilimuuliza mke wake ndugu yangu ananiita kwa room kwa nini na yeye hayuko. Sikujua kwa nini alikuwa ananiita, nilitoka nje tu. Mke wake alikuwa ameenda kazi," Mercy alisimulia.

Aliongeza, "Mke wake alienda kwao lakini saai wamerudiana. Singeweza kuuliza ndugu yangu alitaka nini. Nilikuwa nashuku ndugu yangu. Sasa hivi hashikangi simu zangu. Tuliongea na mke wake mara moja. Nilimpigia kudai pesa yangu."

Lazurus alipopigiwa simu, alibainisha kuwa dadake alimchafulia jina sana na kufanya waliokuwa wamemheshimu wapunguze heshima.

Alisema alijaribu kumtafuta dadake ili wazungumze kuhusu hayo ila Mercy hakuwa anashika simu zake wakati huo.

"Simu zake sijakuwa nikishika kwa sababu kuna wakati nilikuwa namtafuta, hakuwa anashika. Nilikuwa nampigia mara kama ishirini na hashiki. Nikaamua tunyamaziane kama ndio anataka," Lazurus alisema.

Aliendelea, "Mimi kitu nilikuwa namuitia, sio vile alifikiria. Alikuwa anapigia kila mtu akimwambia nilikuwa nataka kumuangukia. Ni kitu yeye mwenyewe alijitungia. Juu aliambia kila mtu akanichafulia jina niliamua tunyamaziane."

Mercy alimuomba kakake msamaha akieleza kwamba alifikiria mambo yake tu.

"Mbona hukuwa unashika simu zangu? Ulikuwa bize ukitangazia kila mtu, hukuwa unataka mambo yangu. Sasa ulikuwa unafikiria nini?" Lazarus alimuuliza dadake.

"Pigia kila mtu uliongea naye uwaeleze kwanza kabla nikusamehe. Kwa sababu uliniharibia jina, na heshima ambayo walikuwa nayo kwangu ilipungua. Ulimpigia mke wangu, alikuja karibu akunywe sumu kwa vitu umejitungia," alimwagiza dadake.

Huku akieleza sababu ya kumuita dadake kwenye chumba cha kulala, Lazarus alisema, "Hiyo nyumba kwanza haina bedroom. Ni single room. Kuna mahali huwa naweka licence, sikuwa naiona. Nilikuwa nataka aondoe vitu vyake ili nitafute. Yeye alifikiria mambo yake akaanza kueneza uongo."

Mercy alisema aliogopa kutii wito wa kakake kwa kuwa walikuwa wao wawili tu kwa nyumba.

"Awapigie awaelezee. Kwa sababu jina liliharibika kabisa nikaanza kuhisi nimekuwa mbaya kabisa. Mpaka mama yangu alikuwa ananiheshimu, saa hii haniheshimu. Saa hii niko na mke mmoja na amenishinda kwa nyumba. Niko na nguvu gani za kujipelekea kwa dadangu... Vile nimemwambia afanye tu hivyo. Akifanya hivyo itakuwa sawa. Na heshima itarudi kama dadangu," Lazarus alisema.

Mercy alisema, "Nitafanya vile anataka lakini alinilaani kwa nini? Hiyo pia ilinishtua. Nitapigia kila mtu, niambia mama."

Je, una maoni ama ushauri gani kuhusu Patanisho ya leo?