Patanisho: Dadangu mkubwa alinitukana nilipokosa kumtumia karo ya mwanangu, Sh300

Nimeishi na mtoto wa Nancy karibu mniaka 6, akiwa darasa la nne mpaka sasa hivi ako kidato cha kwanza. Alimuacha nyumbani akaenda kutafuta kibarua Eldoret." dada mkubwa alifichua.

Muhtasari

• “Mimi nilishamaliza, nilikusamehe sina ubaya na wewe. Ni vile hujanielewa tu lakini mimi nikikasirika ni kwa muda mfupi tu. Mimi nishapoa kabisa.”

GIDI NA GHOST.
GIDI NA GHOST.
Image: RADIO JAMBO

Katika kipindi cha Gidi na Ghost asubuhi kwenye Radio Jambo, mrembo kwa jina Nancy Cheptoo mwenye umri wa miaka 32 kutoka kaunti ya Nandi aliomba kupatanishwa na dadake mkubwa, Celestine Kirui, 38.

Cheptoo alieleza kwamba anahisi alimkosea dadake mkubwa baada ya kujibizana vibaya kuhusu suala la mtoto wake.

Cheptoo alieleza kwamba dadake mkubwa ndiye anamsaidia kumlea mwanaye ambaye alipata akiwa shule.

Dada mkubwa alichukua mwanawe Cheptoo kwa ajili ya kumsaidia katika kumlea baada ya wao kumpoteza mama yao na Cheptoo kuolewa katika ndoa nyingine.

Celestine alimpigia simu akimuomba kutuma pesa Sh300 kwa ajili ya karo ya shule na Cheptoo akamuahidi kufanya hivyo baada ya siku mbili lakini hakufanikisha, jambo lililomkasirisha dada mlezi na kumtumia jumbe za kuudhi.

“Huyu dadangu alichukua mtoto wangu kuishi na yeye, nilipata huyo mtoto nikiwa shule sasa yeye akaamua kumchukua juu tulipoteza mama, juzi akaniitisha pesa ya mtoto, Sh300, nikamwandikia ujumbe nikamwambia sina kwa sasa angoje baada ya siku mbili….”

“Baada ya siku mbili nikamwambia sikupata akakasirika akaanza kunitumia jumbe akinitusi nikamwambia anirudishie mtoto wangu nilee mwenyewe, niko na watoto wengine 2 wadogo ninaishi nao kwangu kwa ndoa,” Cheptoo alieleza.

Dada mkubwa alipopigiwa simu,

“Mimi nilishamaliza, nilikusamehe sina ubaya na wewe. Ni vile hujanielewa tu lakini mimi nikikasirika ni kwa muda mfupi tu. Mimi nishapoa kabisa.”

“Nimeishi na mtoto wa Nancy karibu mniaka 6, akiwa darasa la nne mpaka sasa hivi ako kidato cha kwanza. Alimuacha nyumbani akaenda kutafuta kibarua Eldoret na nikamchukua mtoto wake kutoka nyumbani kumlea,” Celestine aliambia Radio Jambo huku akishukuru kwa kupatanishwa na mdogo wake.