Dennis Murigi ,24, kutoka Nyeri alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mke wake Emily Mukami ,20, ambaye alikosana naye hivi majuzi.
Murigi alisema ndoa yake ya miaka miwili ilisambaratika wiki jana baada ya kutofautiana na mkewe kuhusu suala la simu.
Alisema mkewe alilalamika kuhusu yeye kutochukua simu zake wakati akiwa kazini.
"Mke wangu alikuwa ananipigia simu nakosa kupokea. Wakati mwingine nakuwa bize. Nafanya kazi nakosa muda wa kuchukua simu. Nilijaribu kumweleza mke wangu akauliza kwa nini nakuwa bize kila wakati. Wakati napata muda usiku napata ashalala. Nimeongea na yeye akasema nimpatie muda afikirie," Murigi alisema.
"Sijapigia watu wa kwao. Huwa naskia Patanisho ndiyo poa," aliongeza.
Juhudi za kumpatanisha Murigi na mkewe hata hivyo hazikufua dafu kwani Bi Mukami hakushika simu yake alipopigiwa.
Je, ushauri ama maoni yako kuhusu Patanisho ya leo ni yepi?