Afisa wa jeshi aliyejitambulisja kama Peter Onyango ,31, kutoka Lanet Nakuru alituma ujumbe akiomba kusaidiwa kuokoa ndoa yake ya miaka 9 ambayo inaonekana kuelekea kusambaratika.
Katika ujumbe wake, Onyango alieleza kwamba amekuwa akizozana na mke wake Jackline Alekwa ,29, kwa sababu ya ulevi na anahofia kwamba huenda akatoroka na watoto wao watatu.
Alikiri kwamba kila mara akibugia tembo huwa anakuwa mkorofi na kupeleka hasira yote kwa mkewe.
"Nikinywa pombe nakuwa mkorofi. Nikilewa yeye ndo anakuja adui wangu. Naona amechoka. Naona nimekuwa nikimkosea sana," Onyango alisema.
"Nimeshindwa kuacha pombe sina formula. Hakuna vile naenda rehab, naenda vipi na nitatumia pesa.Haijaharibu maisha, ni ile naona inaniharibia ndoa. Mimi sio Daily Drinking Officer. Lakini ile wakati nakunywa ndiyo nakosea mke wangu. Wakati mwingine najipata nimepigana huko nje. Mke wangu anajaribu kunishauri lakini naona amechoka," aliongeza.
Jackline alipopigiwa simu, alieleza kwamba mumewe amekuwa na mazoea ya kumgeukia kila anapokunywa pombe,
"Atabadilika ama anaomba msamaha alafu arudi vile anakuwanga? Huwa anaomba msamaha leo, alafu kesho anarudia. Nimejaribu kumsaidia, ata nimeambia watu wa kwao, wamejaribu wameshindwa, Nimeambia mama yangu, pia yeye ameshindwa," Jackline alisema.
Onyango alijaribu kujitetea akisema, "Baba alikufa 2021, na yeye ndiye alikuwa rafiki. Niko na kitu inanisumbua, nakosa mtu wa kuambia..Mke wangu, nimeishi kukuomba msamaha kwa simu hadi unachoka. Nisamehe tu, na usichoke kunisamehe."
Aidha, aliahidi kwamba hatakunywa pombe leo kwani hana mshahara.
"Naomba msamaha. Wewe ni mke wangu, tumetoana mbali. Pata mahali kwa moyo wako unisamehe. Ata mimi natamani niache pombe. Usitoroke na watoto wetu," Onyango aliomba.
Jackline alisema, "Kila siku ukipata mshahara, lazima nilie kwa nyumba. Uko na watoto, ujue vile utawaangalia. Ujue vile utaangalia hao watoto, ukishindwa nitajua vile nitawalea pekee yangu
Uskie ushauri, usijifanye unajua kila kitu."
Alionhgeza, "Yeye ndiye baba wa watoto wangu. Kama ameamua kubadilika ni sawa. Sina mpango wa kutoroka."
Je, ushauri ama maoni yako kuhusu Patanisho ya leo ni yepi?