logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Patanisho: "Nampenda, sijawahi kuoa tena!" Jamaa wa miaka 42 aeleza sababu ya kuchumbiana na msichana wa miaka 17

"Nampenda Gidi, nampenda sana. Sikuwahi kuoa tena hapo awali. Tulikuwa sawa mbeleni. Shida ilikuja ikatokea," Baya alisema.

image
na Samuel Mainajournalist

Patanisho28 October 2024 - 08:42

Muhtasari


  • Baya alisema uhusiano wake na Rehema ulisambaratika Desemba 2022 baada ya kutoelewana.
  • "Rehema ujue mimi bado nakupenda, tulikosana na mimi bado nakupenda. Naomba urudi tulee mtoto pamoja," Baya alisema.

Anthony Baya ,42, kutoka kaunti ya Kilifi alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mzazi mwenzake Christine Rehema ,20, ambaye alikosana naye miaka miwili iliyopita.

Baya alisema uhusiano wake na Rehema ulisambaratika Desemba 2022 baada ya kutoelewana.

"Mnamo Desemba 2022, nilikuwa nimeenda kuchukua vitu za mtoto. Kurudi nilipata ameenda kwao. Nimefuatilia, nikafika kwao nikaulizia, ikawa hawezi kurudi kwa sababu kuna mpango alikuwa amefanya na familia," Baya alisimulia.

Aidha, alieleza kwamba familia ya kina mzazi mwenzake tayari imemwambia haitaki mambo yake.

"Kuna vile nilijaribu kugharamia huyo mtoto, shida ikatokea mzazi akasema nisiwe nafika pale kwa sababu huenda kukatokea shida," alisema.

"Katika mila yetu, huwa unapeleka kitu kwa kina yule mwanadada unamchukua. Hivyo ndo nilifanya. Mtoto ana miaka mitatu. Wazazi wanasema nisiende huko," aliongeza.

Aliweka wazi kwamba mpenzi wake alikuwa na miaka 18 wakati alipomtunga ujauzito.

Wakati alipoulizwa kuhusu sababu yake kuingia kwenye mahusiano na msichana mdogo sana kwake, alisema, "Nampenda Gidi, nampenda sana. Sikuwahi kuoa tena hapo awali. Tulikuwa sawa mbeleni. Shida ilikuja ikatokea."

Juhudi za kumpatanisha Baya na mkewe hata hivyo hazikufua dafu kwani Rehema hakupokea simu yake.

Baya alimwambia, "Rehema ujue mimi bado nakupenda, tulikosana na mimi bado nakupenda. Naomba urudi tulee mtoto pamoja."



RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved