logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Patanisho: Mwanadada afichua maelezo ya kushtua kuhusu jinsi ujauzito ulimfanya amchukie mumewe "Sikumpenda, alinuka vibaya!"

"Ilinisumbua sana na yeye hakuweza kunielewa. Nikifua nguo, nafua zangu vizuri na nikifika kwa zake natapika kabisa," Selin alisema.

image
na Samuel Mainajournalist

Patanisho04 November 2024 - 08:38

Muhtasari


  • Selin alisema ndoa yake ya miaka mitatu ilisambaratika Februari mwaka huu wakati alipopata ujauzito wa mtoto wao wa kwanza pamoja.
  • "Vile mimba ilimkataa hivyo, mpaka nikazaa ndo roho yangu ilirudi kwake," Selin alisema.



Selin Achieng .24, kutoka kaunti ya Siaya alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mume wake Richard Omondi ,41, ambaye alikosana naye mapema mwaka huu.

Selin alisema ndoa yake ya miaka mitatu ilisambaratika Februari mwaka huu wakati alipopata ujauzito wa mtoto wao wa kwanza pamoja.

Alisema wakati alipopata ujauzito, alihisi kumchukia mumewe hadi kufikia hatua ya kutoka kwa mumewe na kurudi kwao.

"Vile nilipata mimba, sikuwa nampenda sana, akiingia kwa nyumba naskia ananuka vibaya. Akikaa karibu na mimi naskia tu ananuka vibaya, akitoa nguo yake naskia tu inanuka vibaya. Ata nikimuona naona kama sio mtu, yaani simtaki kabisa," Selin alisimulia.

Aliongeza, "Ilinisumbua sana na yeye hakuweza kunielewa. Nikifua nguo, nafua zangu vizuri na nikifika kwa zake natapika kabisa. Niliona siwezani nikatoka nikaenda. Vile tulipatana naye alikuwa ameoa bibi wengine kama watano hivi wakienda. Hao wenye walienda ni kama hawakuwa wanapata mtoto. Mtoto wa kwanza sio wake, wa pili ndo wake."

Alisema kwamba bado hajaweza kurudiana na mumewe licha ya moyo wake kumkubali tena baada ya kujifungua.

"Hatuko pamoja saai. Vile mimba ilimkataa hivyo, mpaka nikazaa ndo roho yangu ilirudi kwake. Nilimpigia simu nikamueleza, alikasirika kabisa vile nilienda. Nataka nirudi tukae na yeye," alisema.

Richard alipopigiwa simu, Selin aliomba msamaha huku akisisitiza kwamba mimba ndiyo ilifanya awe mkali kwa mumewe.

"Mimba ndo ilinifanya niwe mkali hivyo, haikuwa kupenda kwangu. Baada ya kuzaa ndo nikaona niko tu sawa. Naomba anisamehe, kama tunaweza kurudiana turudiana kama bibi na bwana," alisema.

Richard alijibu, "Sasa ni mpaka nikae chini nifikirie kwa sababu madharau ambayo alinionyesha ni mengi. Alileta kiburi, alinionyesha madharau wakati nilijaribu kumkalisha chini tuongee, akaamua kutoka. Wasichana wa sasa ni ngumu kuwaelewa. Yeye ni mtu ambaye alikuwa akitoka na kurudi ata kabla ya mimba. Ako tu na zake."

Aidha, aliweka wazi kwamba tayari ameoa mke mwingine baada ya Selin kutoroka.

"Anipee muda nitafakari, Niko na mtu mwingine tayari, siwezi danganya. Anipee muda nitafakari la kufanya," alisema.

Selin alisema, "Nampenda kama bwanangu. Yeye ndiye alinioa nikiwa mdogo, saa hii angalau nimekomaa.'

Katika maneno yake ya mwisho, Richard alisema, "Anipee muda natafakari nitamwambia. Akipiga baadaye atapata simu yangu inaingia."

Je, una maoni ama ushauri gani kuhusu Patanisho ya leo?


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved